Marehemu MCD enzi za uhai wake
Historia ya Marehemu Soud Mohammed Timbo (MCD) 1973-2014. Kama
ilivyosomwa na Shemeji yake Bwana Mlanzi siku ya Maziko Jumatano tarehe
29-01-2014.-Marehemu alizaliwa Mwaka 1973 mkoani Kilimanjaro.
-MCD alisoma katika Shule ya Msingi Mawenzi iliyopo Manispaa ya Moshi na alihitimu mwaka 1987. Alianza Masomo ya Sekondari katika Shule ya Shemsanga Korogwe Tanga kuanzia 1988-1992. Baada ya kumaliza masomo ya Sekondari alijiunga na Chuo cha Sanaa Bagamoyo.
-Baada ya kumaliza Chuo cha Sanaa Bagamoyo, alifanya kazi katika Bendi ya Diamond Sound "Wana Dar es salaam Ikibinda Nkoi", African Stars Band "Twanga Pepeta", Mashujaa Musica kwa muda mfupi na baadae alirejea katika Bendi ya African Stars "Twanga Pepeta" mpaka mauti yalipomfika.
-MCD alifunga ndoa na Bi Renada 2001 pia alifunga ndoa na Mwantum Zowo ambaye alikuwa dansa wa Twanga Pepeta na kwa sasa marehemu.
-Marehemu ameacha watoto wanne, wa kike wawili na wa kiume wawili.
-MCD alikuwa ni kijana mcheshi, mpole na kipenzi cha watu msikivu kwa wakubwa na wadogo. Pia alikuwa mwanamuziki mahiri katika upigaji wa Ngoma (Tumba) kwa umahiri mkubwa hakuna mfano wake, ameacha pengo kubwa sana katika Bendi yake ya Twanga Pepeta.
-MCD aliugua kwa muda mfupi na kufariki usiku wa tarehe 27-01-2014 katika Hospitali ya rufaa ya KCMC.
-Familia inatoa shukrani za dhati kabisa toka Mwajiri(Twanga Pepeta), Ndugu, Jamaa na marafiki walioungana pamoja nasi tangu tulipopata msiba huu wa kuondokewa na mpendwa wetu Soud Mohammed MCD.
MWENYEZI TUNAKUOMBA UILAZE ROHO YA MAREHEMU SOUD MOHAMMED SAID TIMBO (MCD) MAHALI PEMA PEPONI- AMEN.
No comments:
Post a Comment