https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Wednesday, January 15, 2014

Rais Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Bilal wawajulia hali Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa David Msuya na Waziri Haroun Ali Suleiman
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Waziri Mkuu Msaafu Mzee Cleopa David Msuya aliyelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili jana jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakimjulia hali Waziri wa nchi Afisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ) Bwana Haroun Ali Suleiman aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam, Jana (Jumanne). Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya, aliyelazwa katika jengo la Moyo Hospitali ya Taifa Muhimbili, wakati alipofika kumjulia hali leo, Jan 15, 2014. Kulia ni mke wa Makamu, Mama Zakia Bilal (kushoto) ni Meneja wa Jengo hilo la Moyo, Sr. Salome Kassanga.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na  Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya, aliyelazwa katika jengo la Moyo Hospitali ya Taifa Muhimbili, wakati alipofika kumjulia hali leo, Jan 15, 2014. Kushoto ni mke wa Makamu, Mama Zakia Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali Waziri wa Kazi na Utumishi wa Umma wa Zanzibar, Haruna Ali Suleiman, aliyelazwa katika jengo la Moyo Hospitali ya Taifa Muhimbili, wakati alipofika kumjulia hali leo, Jan 15, 2014. Katikati ni mke wa Makamu, Mama Zakia Bilal (kushoto) ni Meneja wa Jengo hilo la Moyo, Sr. Salome Kassanga. Meneja wa Jengo hilo la Moyo, Sr. Salome Kassanga.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...