Na Kambi Mbwana, Dar
es Salaam
MAPROMOTA wa mchezo wa masumbwi wameombwa kuwa makini na
waaminifu ili wahakikishe wanasimamia vyema na kuendeleza sekta hiyo ili
kuuletea mafanikio ndani na nje ya nchi.
Hayo yamesemwa na mdau wa ngumi ambaye pia ni jaji wa
masumbwi, Ibrahim Kamwe, alipozungumza na gazeti la Mtanzania Jumapili, ikiwa
ni miezi kadhaa baada ya kudaiwa kuwa muandaaji wa pambano la Francis Cheka na
Phil Williams, ambaye ni Jay Msangi, kulivuruga.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Kamwe alisema kuwa ni wakati wa mapromota
kujitahidi katika maandalizi ya mapambano yao,
sanjari na kuwalipa mabondia na wote wanaostahili ili kuepusha lawama.
“Katika pambano la Cheka na
Williams kulikuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wadau, akiwamo Williams
mwenyewe, hivyo huu ni wakati wa kuliangalia jambo hilo kwa ajili ya kulinda heshima ya mchezo
wa ngumi.
“Tusipokuwa makini hata wale
wachache wanaojituma katika masumbwi watashindwa kuwekeza zaidi kutokana na
imani kuwa mchezo huu unaendeshwa bila kuzingatia vigezo na mahitaji ya
mafanikio yake,” alisema.
Kwa mujibu wa Kamwe, katika pambano
la Cheka na Williams lililolalamikiwa, yeye alikuwa msimamizi mkuu.
No comments:
Post a Comment