Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KATIBU wa Ngumi za Kulipwa hapa nchini, Ibrahim Kamwe, amesema
kwamba mkutano wao utakaofanyika Februari Mosi mwaka Vijana Hall Kinondoni,
utakuwa na faida kubwa ya kujadili sekta hiyo ya masumbwi.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Kamwe alisema kwamba mkutano
huo umepewa Baraka zote na Rais wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa (TPBO),
Yasin Abdallah.
Alisema kuwa anaamini wadau wote wa masumbwi, wakiwamo mapromota
watajumuika pamoja kutafuta namna bora ya kuendeleza mchezo wa masumbwi hapa
nchini.
“Huu ni mkutano wa kwanza unaofanyika nchini huku ukiwa na manufaa
makubwa kwa sisi wadau wa masumbwi hapa nchini, hivyo naomba tujiandaye vizuri
kwa maendeleo yetu.
"Mkutano utaanza mapema asubuhi, huku nikiamini kuwa kila kitu
kitakwenda kama kilivyopangwa, ukizingatia kuwa mbali na mapromota, pia
mabondia na makocha wa ngumi ni miongoni mwa wanaotarajiwa khudhuria,” alisema
Kamwe.
Mchezo wa masumbwi unatajwa kati ya ile iliyopunguza makali yake,
licha ya wadau mbalimbali katika tasnia hiyo kuendelea kuupigania ili ubaki
katika mafanikio yake kama zamani.
No comments:
Post a Comment