https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Friday, January 17, 2014

Chadema nao wapata mwakilishi wa kuwania uwakilishi jimbo la Kiembesamaki, Visiwani Zanzibar

Mgombea Uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar  kupitia Chama cha CHADEMA Bwa. Hashim Juma Issa
Msimamizi wa Tume ya Uchaguzi Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar Suluhu Ali Rashid, akitowa maelezo kwa Mgombea wa CHADEMA Bwa Hashim, alipofika Ofisi za Tume ya Uchaguzi ya Wilaya ya MjiniMagharibi Maisara kuchukua fomu ya kugombea Uwakilishi wa Jimbo hilo lillilokuwa Wazi baada ya Mwakilishi wake kuvuliwa Uwanachama na Chama chake Mhe, Mansoor Yussuf Himid, mwaka jana 
 Msimamizi wa Tume ya Uchaguzi Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar Suluhu Ali Rashid, akimkabidhi Fomu Mgombea wa Uwakilishi wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao.
 Mgombea Uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Bwa. Hashim Juma Issa akisaini baada ya kupokea fomu hizo kutoka kwa Msimamizi wa Tume ya Uchaguzi wa Jimbo la Kiembesamaki Zanzinar

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...