Na Mwandishi Wetu, Oman
KLABU ya Coastal Union jana ilianza
programu ya Gym katika uwanja wa soka wa Sultan Qaboos, jijini Muscat. Coastal
Union ambayo ipo Oman kwa kambi ya wiki mbili kujiandaa na mzunguko wa pili wa
ligi kuu Tanzania bara, imeamua kufanya mazoezi ya gym kuhakikisha wachezaji
wake wanakuwa na misuli imara ili kukabiliana na mikiki ya mechi.
Hafidh Kido, ambaye pia ni msemaji wa Costal Union.
Akizungumza na Handeni Kwetu Blog, kocha wa
Coastal Union, Yusuf Chipo amesema anajua watu wakisikia hivyo wataogopa na
kuanza kuwakamia lakini hana budi lazima afanye hivyo.
"Wewe unanisababishia balaa Tanzania,
yaani najua timu nyingine zikisikia na kuona hivi watakamia, lakini hii ndiyo
hali halisi vijana lazima wapige chuma wawe imara.
"Unajua tumefanya mazoezi mengi uwanani,
gym inasaidia kulainisha na kuifanya misuli kuwa imara. Hii ndiyo njia pekee ya
kuwasaidia," alisema Chipo.
Nae daktari wa timu Dk. Francis Mganga,
amemwambia mwandishi wetu kuwa anafurahi kuona kile kitu alichohitaji kwa
kipindi kirefu sasa kimetimia.
"Hiki niliwashauri viongozi kwa muda
mrefu, wachezaji hawana nguvu, kunyanyua vitu vizito kunaimarisha misuli.
Naamini sasa mambo mazuri, kwasababu hata mchezaji akianguka hawezi kuumia
kizembe ikiwa misuli yake ni imara," alisema.
Katika upande mwingine meneja wa Coastal
Union, Akida Machai aliliambia Raia Tanzania kuwa, atahakikisha ananunua vifaa
vya Gym ili timu iwe na gym yake.
"Gym ni muhimu, hata mimi nimeona,
tutaangalia mfuko wetu umekaaje ili tukirudi tutengeneze gym yetu wenyewe. pale
klabu tuna eneo kubwa tunaweza kununua vifaa na kuanzisha. hata kule kambini
pia tuna vyumba vikubwa," alisema.
No comments:
Post a Comment