Mkuu wa Mkoa Tanga, Chiku Gallawa, pichani.
Na Oscar Assenga, Tanga.IMEELEZWA kuwa uharibifu wa mazingira unaotokana na ukataji miti ovyo,uchomaji wa moto misitu ikiwemo uharibifu wa vyanzo vya maji husababisha kupungua kwa makundi ya nyuki mkoani Tanga.
Kauli hiyo alitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Luteni Mstaafu Chiku Gallawa wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake hivi karibuni ofisini kwake ambapo alisema changamoto nyingine ni uhaba wa maafisa ugani katika mamlaka za serikali za mitaa.
Alisema licha ya kuwa na changamoto hizo uzalishaji wa asali mkoani
hapa umeongezeka kutoka kilo 32,559
mwaka 2011/2012 na kufikia kilo 139,573 Octoba mwaka 2013 wakati
uzalishaji wa nta nao pia umeongezeka kutoka kilo 1886 mwaka 2011/2012
na kufikia kilo 42,000 Octoba mwaka jana.
Mkuu huyo wa mkoa alisema katika mkoa wa Tanga kuna vituo viwili vya
uchakataji wa asali ambapo kimoja kipo
wilayani Lushoto ambacho wanafungasha asali na kutengeneza bidhaa
mbalimbali na kile cha wilayani Mkinga ambacho hakijaanza kutumika
kutokana na uzalishaji mdogo.
Aliongeza kuwa katika mwaka wa fedha 2012/2013 mkoa umefanikiwa
kuanzisha kituo kimoja cha kuchakata
asali kilichopo Kata ya Bungu wilayani Korogwe pamoja na kuongeza
vikundi vya wafugaji nyuki kutoka 264 mwaka 2011/2012 na kufikia 291
Octoba mwaka jana.
Alieleza kuwa katika kipindi cha mwishoni mwa mwaka jana hifadhi mbili
za nyuki zimeanzishwa katika wilaya za Kilindi, Manzuki 12 wilaya ya Mkinga na mbili wilaya ya Korogwe.
Alisema kupitia wakala wa misitu Tanzania mkoa umegawa mizinga ya
kisasa 100 kwa kila halmashauri kwa
lengo la kuongeza hamasa ya wananchi kufuga nyuki ikiwemo kuzitaka
kuhakikisha kila kikundi cha ufugaji kinafikisha idadi kama hiyo
ilianishwa badala ya 12 ya sasa ili kupata faida.
Hata hivyo alisema mkoa ulitumia maonyesho ya Kimataifa ya Biashara na
Kongamano la Uwekezaji Kanda ya
Kaskazini yaliyofanyika mkoani hapa kama fursa kwa wafanyabishara na
wajasiriamali wa mazao yanayotokana na ufugaji wa nyuki kuonyesha bidhaa
na huduma zao ili kupanua masoko
ndani na nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment