https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Thursday, January 16, 2014

DAWASCO nao wataja wadeni wao kuwa ni Bilioni 40

http://4.bp.blogspot.com/-g1Fpf0dF-oY/UtbmdQAU1JI/AAAAAAAFHE4/Mbj9ID093ws/s1600/DSC_0035.JPGAfisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO Eng Jackson Midala akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya matukio mbalimbali ya shirika lake kwa mwaka 2013 na mategemeo ya uboreshaji huduma kwa mwaka 2014. Kulia ni Ofisa Uhusiano wa Dawasco, Everlasting Lyaro.
 
Shirika la majisafi na majitaka Dar es salaam(DAWASCO) imesema inawadai wateja sugu Tsh 40 bilioni huku ikiwataka kulipa madeni ili kunusuru utendaji wa shirika.

Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya DAWASCO kukatiwa huduma ya umeme na TANESCO kutokana na deni la sh 6.3.

Hayo yamesemwa na afisa mtendaji mkuu wa DAWASCO, Eng Jackson Midala alipokuwa anaongea na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki.

Alisema mamlaka hiyo imeshindwa kulipa kulipa deni hilo kwa wakati kutokana na kuwadai wateja wake zikiwemo taasisi za serikali zaidi ya bilion 40.alisema deni hilo linahusisha baadhi ya taasisi za serikali na watu binafsi.
“kuna hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Jeshi la Wananchi wa Wanzania (JWTZ), Polisi na wengine wengi.hatuwakatii huduma kwa sababu ya madeni ila tunasisitiza kulipa madeni hayo ili na sisi tuweze kulipa mzigo wa madeni mengine ya umeme” alisema Midala
Alisema “hivi karibuni mtambo wa ruvu juu uliharibika na mafundi wetu walifanikiwa kuutengeneza, lakini siku ya jumamosi umeme wa TANESCO ulikatwa kwasababu ya deni, jambo lililosababisha Maji kukatika tena kwenye sehemu nyingi za jiji la Dar es salaam”
Pia midala alisema kuhusu hatua zinazoendelea kuwashughulikia wateja wanaoiba Maji kwa njia za kuharibu mita kwamba mpaka sasa wamewakamata watu 284 na kuwafikisha mahakamani.

Alisema miongoni mwa watu hao, watatu walihukumiwa adhabu ya kifungo, watatu kesi zilifutwa kwa kukosa ushahidi na wengine kesi zao zinaendelea.
Aliwataka wateja kulipa Ankara zao kwa muda, lengo likiwa kuwezesha mamlaka hiyo kujiendesha na kuendelea kuwapa huduma na pia kutoa taarifa za wizi wa Maji na uharibifu wa miundo mbinu kupitia simu yake ya Mkononi 0779-090900.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...