Na
Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BENDI
ya Mapacha Watatu, inajivunia kumaliza mwaka 2013 kwa kufanya matukio manne
makubwa na kudhihirisha ubora wao katika tasnia ya muziki wa dansi hapa nchini.
Vijana wa Mapacha Watatu pichani.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam, Meneja wa bendi hiyo, Khamis Dacota, alisema kwamba
matukio hayo yaliandaliwa kwa ubora bila kuangalia changaamoto zozote
wanazokutana nazo.
Alisema
mwaka huo wa 2013 uliomalizika waliweza kuzindua albamu yao ya Yarabi Nafsi,
Cindy VIP Show, Kumbukumbu ya kuzaliwa Mapacha Watatu pamoja na tukio la
kumkaribisha mwimbaji wao Catherine Cindy kutoka ughaibuni.
“Haya
ni mafanikio makubwa ambayo tuliweza kuyaandaa kwa kiwango cha juu na
kudhihirisha ubora wetu katika tasnia ya muziki wa dansi hapa nchini, licha ya
kukabiliwa na changamoto kadhaa.
“Naamini
mwaka huu utakuwa mzuri zaidi kwa upande wa Mapacha Watatu, sanjari na
kuendeleza makali yetu kwa kushirikiana na wadau wote wanaotuunga mkono,”
alisema.
Kwa
mujibu wa Dacota, wanamuziki wake wamejipanga imara kuendeleza burudani kwa
mashabiki wao kwa ajili ya kuwa kileleni kwa kushindana na bendi mbalimbali
zinazofanya vizuri hapa nchini.
No comments:
Post a Comment