Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
ALIYEKUWA kocha msaidizi wa klabu ya Yanga, Fredy Minziro,
amesema kwamba hatishwi na uamuzi wa kuachwa kwake katika benchi la ufundi la
timu hiyo, kwasababu anaamini ujuzi wake atapata sehemu kwa kuupeleka.
Fredy Felix Minziro, aliyekuwa kocha msaidizi wa Yanga
Maneno ya Minziro yamekuja baada ya Yanga kutimua benchi lote
la ufundi, ikiwa ni mwendelezo baada ya kumuacha Kocha wao Mkuu, Ernest
Brandit.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Minziro, alisema kuwa
amekuwa akivunja ujuzi mwingi kutoka kwa makocha mbalimbali waliopita Yanga
katika kipindi cha miaka minne, huku akiwa kama kocha msaidizi.
Alisema jambo hilo linampa matumaini makubwa kuwa uwezo wake
umekuwa mkubwa na hawezi kukosa timu ya kuifundisha atakapoona inafaa, hivyo
hana shaka na uamuzi wa mabosi wake.
“Siwezi kuumizwa na hatua hii ya kuachwa Yanga, ukizingatia
kuwa sijaona tatizo langu wala kupewa sababu ya kueleweka kwanini benchi la
ufundi linaachwa bila sababu za msingi.
“Hata hivyo kwakuwa wao ndio wameamua, nimepokea uamuzi huo
kwakuwa nitakapoamua kusaka timu ya kufundisha siwezi kukosa kutokana na ujuzi
wangu niliyokuwa nao,” alisema Minziro.
Uamuzi wa Yanga umekuja huku ukipokewa kwa shingo upande na
mashabiki wao, ikiwa ni siku chache kabla ya kuanza kinyang’anyiro cha
mzunguuko wa pili wa ligi ya Tanz
No comments:
Post a Comment