Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KUNDI la Jahazi Modern Taarab limefafanua ni kwanini
limeamua kuuchagua mji wa Morogoro kama kituo chao cha kwanza cha kutambulishia
nyimbo zao mpya zitakazounda albam yao mpya ijayo.
Mauaji akizungumza na mwanadada Hawa Hassan kulia kwake.
Jahazi wanatagemewa kufanya onyesho maalum Morogoro kwaajili
ya kuwaonyesha nyimbo mpya mashabiki wao Ijumaa ya tarehe 31 mwezi huu ndani ya
ukumbi wa Tanzanite Complex.
Jana kiongozi wa Jahazi Modern Taraab Mohamed Mauji alifanya
mahojiano na kipindi cha Sham Sham za Pwani cha ITV kinachoongozwa na
mtangazaji Hawa Hassan (Kama wanavyoonekana pichani) ambapo msanii huyo alitoa
sababu kadhaa ni kwanini wameichagua Morogoro. Kipindi hicho kitaruka hewani
Jumamosi hii saa 11 jioni.
Mauji ambaye ni mcharazaji gitaa la solo miongoni mwa sababu
nyingi alizozitoa ni pamoja na kusema kuwa mji wa Morogoro ni ngome yao kubwa
(ukiondoa Dar es Salaam) na hivyo safari hii wameupa heshima ya kipekee.
Mara zote Jahazi imekuwa ikianza kutambulisha nyimbo mpya
jijini Dar es Salaam na baadae kufuatiwa na uzinduzi na baada ya hapo ndio
wanazipeleka nyimbo mpya mikoani.
Mauji pia katika mahojiano yake hayo alifichua mikakati yao
mikubwa ya kukukabiliana na ushindani kwa mwaka huu wa 2014.
No comments:
Post a Comment