https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Monday, January 13, 2014

Dayna Nyange: Mungu ni kila kitu kwanguNa Kambi Mbwana, Dar es Salaam
NYOTA wa muziki wa kizazi kipya maarufu kama Bongo Fleva, Mwanaisha Said ‘Dayna Nyange’, amesema mafanikio yake yapo mikononi mwa Mungu, anayejua kumuongoza katika sanaa yake.
Dayna Nyange pichani.
Hiyo ni kauli nzito kwa mwaka huu ya mwanadada huyo, ambaye amefanikiwa kuachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Mimi na Wewe’, ulioanza kufanya vizuri katika vituo vya redio hapa nchini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Dayna alisema alianza katika hatua ya chini akivumilia mikiki mikiki ya kila aina, ila leo amejiweka katika nafasi nzuri kutokana na njia nzuri anayopita.

“Mungu wangu ndio kila kitu katika maisha yangu ya muziki hapa nchini, hivyo daima nitaendelea kumuomba yeye ili nisiweze kushuka na kuwaangusha mashabiki wangu, ambao tangu mwanzo nao wananipa ushirikiano.

“Tangu natoka na wimbo wa Mafungu ya Nyanya nikiimba na msanii Lawrence Malima, maarufu kama Marlaw, sijaweza kuwa katika mazingira magumu zaidi, hivyo naamini hii yote ni mipango ya Mungu muweza wa yote,” alisema Dayna Nyange.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...