Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
RAIS wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Jamal Malinzi,
amesema msimu ujao wa ligi watakaa ili kuuboresha zaidi, ikiwa ni pamoja na
kurudisha mtindo mechi zote za Ligi Kuu kutanguliwa na mechi za vijana.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi, pichani.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana Malinzi
alisema mtindo utaongeza ufanisi na ushindani katika patashika ya ligi ya
Tanzania Bara, huku wakiamini kuwa mpango huo utakuwa na tija kwa sekta ya
mpira wa miguu.
Alisema kuwa mara baada ya ligi hii ambayo hatua ya mzunguko
wa pili itaanza Jumamosi hii, watakaa na wenzake kulipitisha wazo hilo kwa
ajili ya kutafuta fursa ya kukuza mpira wa miguu.
“Tutajaribu kuliangalia wazo la mechi za ligi zote
kutanguliwa na mechi za vijana katika viwanja vyote, tukiamini kuwa utakuwa ni
mpango mzuri wa kukuza soka la letu, badala ya kusubiri Uhai CUP tu.
“Naamini tutafanikiwa kwa pamoja ukizingatia kwamba tumeingia
katika mchakato wa kila mmoja wetu kuhakikisha kuwa anatimiza wajibu wake na
kufanikisha maendeleo ya mchezo huo nchini,” alisema.
Malinzi ameingia madarakani katika ofisi za TFF kama rais,
akirithi mikoba ya Leodgar Tenga, aliyemaliza muda wake.
No comments:
Post a Comment