Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
RAIS wa
Shirikisho la Soka nchini (TFF), Jamal Malinzi, amesema kwamba kuna kila sababu
ya kuweka mkazo kuweka program nzuri za kuendeleza soka la vijana ili iwe
chachu ya kuendeleza mchezo huo.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi, pichani.
Akizungumza mapema
wiki hii, Malinzi alisema kwamba juhudi za kuendeleza mpira wa miguu zitakwamua
na kuleta mafanikio makubwa katika tasnia hiyo.
Alisema kuwa
juhudi hizo pia zinaweza kwenda sambamba kwa kuanzia pia kwenye shule
mbalimbali, ukizingatia kuwa huko ndipo kwenye watu wanaostahili kuanza kucheza
soka.
"Hii
itatusaidia kwa kiasi kikubwa kwakuwa ndio msingi imara wa kukuza sekta ya
mpira wa miguu, ukizingatia kuwa ndio sera nzuri tunayohitaji kuisimamia kwa
vitendo,” alisema.
Wakati
anafanya kampeni za kumuingiza madarakani, rais Malinzi ilikuwa ni ajenda yake
kubwa ya kuwa na ndoto ya soka la vijana, ikiwapo kuandaa mashindano ya vijana
Barani Afrika, katika ardhi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment