https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Tuesday, January 14, 2014

FM Academia waenda mikoani kuinadi Chuki ya Nini

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

BENDI ya Muziki wa dansi ya Extra ya FM Academia inatarajia kuipeleka albamu yao ya 10 ya Chuki ya nini waliyoizindua hivi karibuni Dar es Saalam mikoa nane zaiara inayotarajia kuanza mapema mwezi Februari mwaka huu.
Rais wa bendi ya FM Academia, Nyosh El Sadaat.
Mikao ambayo wanatarajia kufanya maonesho hayo ni Mwanza, Mbeya, Songea, Kilimanjaro wilayani Moshi, Arusha, Morogoro, Tanga na Dodoma.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa fedha na utawala wa bendi hiyo Kelvin Mkinga alisema, lengo la kufanya ziara hiyo ni kutaka kuwapa ladha halisi ya albamu ya albamu hiyo kama ilivyokuwa kwa wakazi wa Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kuwatambua wanamuziki wao.

“Tunataka albamu hii mashabiki wetu waitambue na wapate ladha halisi  hivyo wakae tayari kwa maonesho yetu mikoa hiyo na tunawaahidi kuwapa shoo ya nguvu ingawa bado hatuja panga mkoa ambao tutaanza nao,” alisema.

Kelvin alisema, kwa sasa wapo katika mazungumzo na moja ya kampuni za usmabazaji ili waweze kuwasambazia albamu yao hiyo ambapo wanahitaji kampuni ambayo ambayo itakuwa na faida kwao na kwa manufaa ya wanamuziki.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...