https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Thursday, January 02, 2014

Clouds Media Group waadhimisha miaka 14 kwa kuwajulia hali wagonjwa na kuwapa msaada Hospitali ya Temeke




 Mtangazaji wa kipindi cha Clouds FM, Dr Isaac Maro akikabidhi msaada wa vifaa kwa Dr Muzdalifat Abeid, bingwa wa magonjwa ya wanawake na uzazi hospitali ya Temeke, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 14 ya Clouds FM.
 Mtangazaji wa kipindi cha Clouds FM, Dr Isaac Maro akikabidhi msaada wa vifaa kwa Dr Muzdalifat Abeid, bingwa wa magonjwa ya wanawake na uzazi hospitali ya Temeke, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 14 ya Clouds FM.

KITUO cha Redio namba moja hapa nchini, Clouds FM kimefikia kilele cha mwezi wa maadhimisho ya miaka 14 toka kimeanzishwa. Maadhimisho hayo ambayo yamefanyika kwa mwezi mzima sasa, yalianza na watangazaji  wa vipindi tofauti kwenda mikoa mbalimbali ili kuweza kusherekea miaka  hii 14 pamoja na wasikilizaji wao sehemu walipo.

Ikiwa ndio siku ya kilele cha maadhimisho hayo, Clouds FM imetembelea
hospitali ya Temeke na kituo cha kuhudumia vijana wanaotumia madawa ya  kulevya cha Keko Youth, ambapo misaada mbalimbali imetolewa. 
Wakiwa katika hospital ya Temeke, Clouds FM imetoa vifaa mbalimbali vya  hospitali katika wodi ya wanawake na watoto, huku Keko Youth wakipewa  vitendea kazi ambavyo vitawezesha vijana kujiajiri baada ya kumaliza  matibabu.

Akizungumzia maadhimisho hayo ya Clouds FM, Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media  Group, Joseph Kusaga alisema sherehe hizi kwa mwaka huu ni za kipekee  kwa Clouds FM hasa kwa kuwa wameweza kufanikisha  mambo mengi makubwa  toka walipoanza. ‘Maadhimisho  haya ya miaka 14 kwa mwaka huu yana lengo moja kubwa, kuwashukuru  wasikilizaji wetu kwa kutufikisha hapa tulipo, na ndio maana tumeanza  kwa kuwapa misaada wanaohitaji, halafu tunamalizia kwa burudani’’  alisema Kusaga.
Akielezea zaidi mafanikio ya Clouds FM kwa kipindi cha miaka 14, Kusaga alisema  redio imefanikiwa kuwafikia watu wengi zaidi, imeongeza ubunifu lakini  pia kumekuwa na uboreshaji wa hali ya juu wa mitambo ya kutangazia  pamoja na maudhui.

‘Kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo tumefanikiwa kushinda tuzo ya Super  Brand, na kwa mwaka huu pekee radio imefanikiwa kuanza kusikika mikoa ya Njombe, Songea, Njombe, Sumbawanga, Katavi na Geita, kupitia mitandao  kwa wasikilizaji wetu nje ya nchi lakini pia tumefanikiwa kufanya
tamasha la Fiesta kwa mafanikio zaidi’ alisema Kusaga.

Kusaga pia aligusia mchango wa Clouds FM katika kuhamasisha maendeleo na  uzalendo hapa nchini akitoa mfano wa semina za Fursa ambazo zilifanikiwa kwenda nchi nzima zikizungumza na vijana kuamka na kuchangamkia fursa  katika sehemu wanazoishi. ‘Semina za Fursa zimekuwa mfano mkubwa namna Clouds FM ilivoweza kutumia nguvu  yake kama radio inayosikilizwa zaidi katika kuchagiza maendeleo, na kwa  hakika mafanikio ya semina yamekuwa ni makubwa sana’ alisisitiza Kusaga.
  
Kusaga pia alitoa shukrani za pekee kwa watanzania kwa kuinga mkono Clouds FM  sio kwa kusikiliza tu bali hata katika kuhudhuria matamasha na shughuli  nyingize za Clouds. Kilele cha  maadhimisho ya miaka 14 ya Clouds FM kitamalizika kwa burudani kubwa  ambayo itafanyika katika viwanja vya Mwembeyanga ambayo itajumuisha  wasanii na watu wengine maarufu.
‘Kumekuwa na mafanikio makubwa katika redio yetu kwa kipindi cha miaka 14, na  naomba niseme, bila ninyi wasikilizaji wetu tusingeweza kufika hapa’  alimaliza Kusaga
 Mtangazaji wa Kipindi cha Power Breakfast, Paul James (PJ), akikabidhi msaada wa pedi kwa mmoja wa wakina mama walio katika wodi ya wazazi wa hospitali ya Temeke.
 Msanii wa mashairi na kughani, Mrisho Mpoto akikabidhi msaada wa pedi za watoto kwa Mama Leah Othman katika hospitali ya Temeke ikiwa ni katika kuadhimisha miaka 14 ya Clouds FM.
 Mtangazaji wa Jahazi, Ephraim Kibonde akimfariji mmoja wa akina mama katika wodi ya wazazi katika hospitali ya Temeke.
 Mtangazaji wa kipindi cha Ampilifaya, Millard Ayo akimhoji mmoja wa vijana ambao wameacha kutumia madawa kwa msaada wa kituo cha Keko Youth. Clouds FM ilitembelea kituo hicho ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 14 na kutoa msaada wa mashine ya kupaka rangi kwa vijana hao
 Baadhi ya wafanyakazi wa Clouds FM wakiwa katika picha ya pamoja na wanawake waliokuwa katika wodi ya watoto katika hospitali ya Temeke, baada ya kukabidhi misaada yao ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 14 ya Clouds FM.
 Mtangazaji wa kipindi cha Ampilifaya, Millard Ayo akiwa amempakata mtoto, baada ya kutembelea hospitali ya Temeke na kukabidhi misaada ikiwa ni sehemu ya miaka 14 ya Clouds FM.
 Mtangazaji wa kipindi cha Club 10, Perfect Chrispin akikabidhi michango ya papo kwa papo iliyotolewa na wafanyakazi wa Clouds FM kwa kituo cha mwanzilishi wa kituo cha Keko Youth, Yohana Victor Haule. Mbele yao ni mashine ya kupaka rangi iliyotolewa na Clouds FM kama msaada kwa kituo hicho.
  Mwanzilishi wa kituo cha Keko Youth, Yohana Haule akimkabidhi zawadi ya kuku Meneja wa Vipindi wa Clouds, Seba Maganga, ikiwa ni kama shukrani kwa kutembelea kituo chao.
=========  ======= ========

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...