https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Thursday, January 23, 2014

Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye atembelea Clouds Media Group na kuzungumza na wadau mbalimbali katika redio hiyo

 Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akimkaribisha Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye alipowasili mapema leo kwenye makao makuu ya ofisi hizo zilizopo Mikocheni jijini Dar,pichani kati anaeshuhudia ni Ofisa Mahusiano wa Clouds Media Group,Simon Simalenga.
  Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akitoa maelezo mafupi kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye kwenye moja ya Ofisi za kampuni hiyo,alipofanya ziara fupi mjengoni humo na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo zikiwemo  na urushaji wa matangazo ya redio na Televisheni kwa ujumla. pichani kati anaeshuhudia ni Ofisa Mahusiano wa Clouds Media Group,Simon Simalenga.
 Mkuu wa Kitengo cha Habari Clouds FM,Joyce Shebe akitoa ufafanuzi mfupi  kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye alipotembelea kitengo hicho cha habari na kujionea uandaaji wa habari ya televisheni na redio unavyofanyika.
 Mmoja wa Watangazaji kipindii cha Michezo Clouds FM,kiitwacho Sports Extra, Ibrahim Masoud a.k.a Maestro akifanya mahojiano mafupi na Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye kuhusiana ushabiki wake mkubwa kwa timu ya Simba sambamba na migogoro iliyoikumba club hiyo ya Msimbazi.
 Ruge Mutahaba akitoa ufafanu mfupi kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye,kuhusiana na Kifaa maalum na cha kisasa cha kurushia matangazo ya biashara,pichani nyuma ni Mkuu wa Kitengo cha Habari Clouds FM,Joyce Shebe akisikiliza.
 Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye akiwa kwenye chumba cha kurekodia mahojiano mbalimbali, akiwa amekutana na wadau wa Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT), pichani kulia ni Afisa Masoko Mwandamizi wa UTT,Mfaume Kimario na Afisa Masoko na Uhusiano,Bwa.Rahim Mwanga
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akitoa maelezo mafupi kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye kuhusiana na urushaji wa matangazo kwa njia ya kisasa ndani ya studio kuu ya redio Clouds FM,Sumaye amefanya ziara fupi mjengoni humo na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo zikiwemo  na urushaji wa matangazo ya redio na Televisheni kwa ujumla. 
Ruge Mutahaba akimtambulisha Mkurugenzi mwanzake wa Maendeleo ya Biashara,Sheba Kussaga kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Mh.Frederick Sumaye
Mkuu wa Kitengo cha uzalishaji vipindi wa Clouds TV, Bwa Kanyopa akitoa ufafanuzi mfupi kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Mh.Frederick Sumaye namna ya kuandaa na kuhariri vipindi vya televisheni.
Ruhe Mutahaba akitoa maelezo mafupi kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Mh.Frederick Sumaye kuhusiana na mitambo ya kisasa ya kurushia matangazo ya televisheni na ubora wa picha za televisheni unaotoka kwenye mitambo hiyo ya kisasa. PICHA ZOTE NA MICHUZIJR WA MICHUZI MEDIA GROUP

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...