Naibu
Waziri Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiongea na Kamati za
Ulinzi na Usalama za Mikoa ya Manyara na Dodoma wakati wa kikao maalum
cha kujadili masuala ya migogoro ya mipaka katika Hifadhi ya Taifa
Tarangire na Pori la Akiba la Mkungunero wilayani Babati, Manyara.
Mkuu
wa Mkoa wa Manyara Mhe. Elaston Mbwilo akisitiza jambo wakati wa kikao
maalum cha Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Dodoma na Manyara
cha kujadili masuala ya migogoro ya mipaka katika Hifadhi ya Taifa
Tarangire na Pori la Akiba la Mkungunero wilayani Babati, Manyara. Kulia
ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi.
Sehemu
wa wajumbe waliokutana katika kikao maalum cha Kamati za Ulinzi na
Usalama za mikoa ya Dodoma na Manyara cha kujadili masuala ya migogoro
ya mipaka katika Hifadhi ya Taifa Tarangire na Pori la Akiba la
Mkungunero wilayani Babati, Manyara.
Kutoka
kulia: Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi, Mkurugenzi wa Idara ya
Wanyamapori Profesa Alexander Songorwa na KatibuTawala wa Mkoa wa
Dodoma Rehema Madenge wakifuatilia mada zilizowasilishwa wakati wa kikao
maalum cha Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Dodoma na Manyara
cha kujadili masuala ya migogoro ya mipaka katika Hifadhi ya Taifa
Tarangire na Pori la Akiba la Mkungunero wilayani Babati, Manyara.
Naibu
Waziri Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiongea na Waheshimiwa
Wabunge Zabein Mhita na Moza Abeid kutoka Dodoma wakati wa kikao hicho.
Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiongea na wanahabari mara baada ya kikao hicho.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu Serikali
ameagiza kumalizwa kwa migogoro ya mipaka baina ya Hifadhi ya Tarangire,
Pori la Akiba la Mkungunero na wananchi iliyodumu kwa muda wa
takribani miaka kumi hadi sasa. Nyalandu amewataka wananchi wa vijiji
vinavyopakana na hifadhi hizo kuacha kuvamia maeneo yaliyotengwa
kisheria kwani kwa kufanya hivyo ni kuleta migogoro isiyo ya lazima. Mhe. Nyalandu alikuwa akiongea katika kikao maalum cha Kamati za Ulinzi na
Usalama za mikoa ya Manayara na Dodoma wilayani Babati mkoani Manyara zilizokutana kwa ajili ya kujadili suluhu ya migogoro hiyo. Aliongeza kusema kuwa serikali imedhamiria kumaliza mgogoro hiyo kwa kuishirikisha jamii kwa upana zaidi huku akisisitiza kwamba Serikali itaendelea kusimamia na kutekeleza Sheria ya Uhifadhi bila kumuonea mwananchi yoyote na kwa kuzingatia haki za binadamu.
No comments:
Post a Comment