Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKOA wa Morogoro umetajwa kama ngome ya kundi la Jahazi
Modern Taarab, hali inayowafanya mashabiki wakanyagane kila linapofanya shoo
mkoani humo.
Mzee Yusuph pichani, akicharaza kinanda.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mdau wa muziki wa
taarabu, ambaye pia ni Mratibu wa shoo ya Jahazi iliyopangwa kufanyika Januari
31 katika Ukumbi wa Tanzanite Complex, Warda Makongwa, alisema watu wa Morogoro
wanaipenda sana Jahazi.
Alisema ingawa kundi hilo pia linaheshimika katika mikoa
mbalimbali ya Tanzania, lakini kwa Morogoro ni miongoni mwa ngome zao hapa
nchini.
“Heshima kubwa ya Jahazi imejikita kwa mkoa wa Morogoro,
hivyo tunaamini kwa pamoja tutaufungua mwaka huu kwa burudani za aina yake
kutoka kwa Jahazi.
“Kila kitu kipo sawa kuonyesha burudani za ukweli kutoka kwa
Jahazi chini ya Mzee Yusuph, hivyo tunaomba wadau waje wka wingi katika Ukumbi
wa Tanzanite,” alisema Warda.
Kwa mujibu wa Warda, maandalizi ya safari ya Jahazi kwa mkoa
wa Morogoro yamekamilika, hivyo wadau wanapaswa kujiandaa na kujivunia burudani
ya Jahazi.
No comments:
Post a Comment