Na Kambi Mbwana, Dar
es Salaam
KOCHA wa mchezo wa masumbwi nchini, Rajabu Mhamila ‘Super D’
amesema kuwa lengo la kuamua kutengeneza CD zinazochanganya mapambano ya
mabondia mbalimbali ni kuongeza chachu ya vijana kujiingiza katika tasnia hiyo
inayosua sua kwa sasa.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, alisema kuwa CD hizo za
masumbwi zinaweza kuongeza hamasa ya wakubwa na wadogo kupenda kucheza ngumi
kwa kuona mapambano hayo.
“Mchezo wa masumbwi kwa Tanzania umekuwa ukisua sua mno,
hivyo tangu mwanzo nikaamua kuja na wazo hili ambalo kwa kiasi kikubwa linatoa
fursa nzuri kwa wadau wote.
“Nawaomba wadau na mashabiki waweze kupata CD hizi katika
mapambano mbalimbali yanayofanika nchini, huku CD hizo zikionyesha picha halisi
ya wakali wa masumbwi ndani na nje ya nchi,” alisema Super D.
Mbali na shughuli hiyo ya kutengeneza CD, Super D ni kocha
wa masumbwi anayetokea katika club ya Ashanti
yenye maskani yake Ilala, jijini Dar
es Salaam.
No comments:
Post a Comment