https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Tuesday, January 21, 2014

Maji ya visima vilivyochimbwa wilayani Muheza yathibitishwa kuwa na ubora


Na Hadija Bagasha, Muheza
MAABARA  ya kupima ubora wa maji Mkoani Tanga imesema kuwa visima tisa vya maji vilivyochimbwa katika mji mdogo wa Muheza maji yake yameonekana kuwa na ubora mzuri na kubainika kuwa yanafaa kwa matumizi ya binadamu.

Taarifa hiyo ilitolewa na Kaimu Meneja wa Maabara ya Maji mkoa wa Tanga Rukia Tuwano na kupewa nakala Mbunge wa jimbo la Muheza Herbert Mntangi.

Alisema kuwa kazi hiyo ya vipimo vya maji imegharimu shilingi 1848000 na  kueleza kuwa uchunguzi wa ubora wa maji umefanyika na kilichogundulika ni kwamba maji kutoka katika vyanzo vyote vya visima tisa yanafaa kwamatumizi ya nyumbani.


Tuwano alisema kuwa visima viwili ambavyo ni cha Michungwani  Tank na  Michungani kwa Mafua vimeonekana ni safi kwa kutokuwa na Bacteria huku visima saba vimeonekana kuchafuliwa na Coliform bacteria na kusema kuwa visima hivyo vinatakiwa kuwekwa dawa ya kuulia  Bacteria hao.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Muheza Herbert Mntangi alisema kuwavisima hivyo tisa vinne vipo maeneo ya  Genge na  vitano vipo maeneo ya Lusanga.

Mntangi alisema kuwa kwa taarifa hiyo sasa kamati ya madiwani ya

Elimu,Afya na Maji baada ya kupokea taarifa hiyo toka kwake Mbunge imeagiza ununuzi wa Pampu kwa visima vya Michungwani Tank na Michungwani kwa Mafua ili wananchi waweze kufaidika na huduma hiyo.

Mbunge huyo aliagiza ununuzi huo ufanyike haraka ili huduma hiyo ya maji  iweze kupatika na wilayani hapo kwa lengo la kupunguza changamoto kubwa ya majini inayowakabili wakazi wa Muheza.


Mntangi aliwahakikishia wajumbe wa kamati hiyo katika kikao
kilichofanyika juzi ukumbi wa Bomani wilayani Muheza kwamba
zitapatikana fedha shilingi 273’000 000 wiki hii na kazi itaanza mara moja  huku wakisubiri ahadi ya shilingi Bilioni 1 iliyotolewa na Waziri wa maji Jumanne Maghembe  ambayo itasaidia kusambaza miundo mbinu ya maji Muheza mjini.


Alisema kuwa visima hivyo viwili vinatoa maji mengi lita Laki nne kwasiku moja ambapo visima vyote tisa  vikikamilika kuwekwa pampu vitatoa Lita Milioni 1.6 kwa siku ambapo shida ya maji itapungua mji wa Muheza wakisubiri mradi mkubwa wa mto Zigi ambayo ni ahadi ya Rais Jakaya Kikwete.


Mntangi alisema kuwa kata ambazo zitafaidika na mradi huo wa visima tisa ni  Majengo’ Genge,Mbaramo, Tanganyika,Masuguru’ Lusanga,Kwamkabarana Michungani na kwamba endapo fedha zitapatikana shida ya maji Muheza mjini itakuwa imeisha.

Mtangi alikemea tabia ya kuchezea fedha za miradi kama hiyo zinapokuja  halmashauri kama zamani zaidiya shilingi Milioni 150 wamenunua mabomba na koki mbovu huku fedha zilizobakia wamekula ambapo Mwenyekiti wa halmashauri ya Muheza Amiri Kiroboto alithibitisha hilo.

Alisema kuwa kwa upande wa miradi ya maji vijijini tayari wametekeleza mradi wa Ubembe maji yanatoka na watayafikisha vijiji vya Misongeni mpaka Mikwamba yataungana na mradi mkubwa wa Magoroto yatakwenda mpaka Muheza mjini.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...