Na Mwandishi Wetu, Pangani
TIMU ya Soka la APL kutoka Kata ya Mwera, imetoka kifua
mbele huku wakitangazwa mabingwa wapya wa kombe la Mwidau CUP.
Timu hiyo iliibuka na ushindi dhidi ya timu ya Torino ya
mjini Pangani, ambayo ilishindwa kufua dafu kwa kufungwa kupitia penati.
Mbunge Amina Mwidau, akimkabidhi kikombe cha ushindi
Nahodha wa timu ya APL Mwera Shabani Athuman, baada ya timu hiyo kutawazwa kuwa
mabingwa wa ligi ya Mwidau CUP, mjini Pangani jana.
Hadi dakika tisini za mchezo huo wa fainali hiyo ya Mwidau
CUP zinamalizika timu zote zilishindwa kutambiana na kulazimika kutoka suluhu
ya bao 1-1.
Kutokana na hali hiyo timu hizo ilizilazimu kuingia katika
hatua ya matuta ambap kati ya penati nne zilipingwa kwa kila timu, Torino
ilipoteza penati mbili huku APL Mwera ilipoteza moja hali hiyowafanya kuibuka
na ushindi na kutawazwa mabigwa wa ligi hiyo.
Timu hizo hadi zinakwenda mapumziko katika kipindi cha
kwanza kila timu ilitoka huku ikishindwa kuona nyau ya mwenzake lakini
ilipofika dakika ya 57, mchezaji Christopher Gunda wa APL alifanikiwa kuziona
nyavu za Torino.
Hata hivyo katika dakika ya 62 Torini ilijibu mapigo na
kusawazina bao hilo ambapo hadi dakika 90 timu zote zilishindwa kutambiana na
kuamua kupigwa matuta.
Awali akihutubia kabla ya kuanza kwa mchezo huo mgeni rasmi
katika mashinda hayo ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga, Amina
Mwidau (CUF), aliwataka vijana kuthamini michezo kwani ajira ambayo imekuwa na
manufaa kwa Taifa.
“Kwa imani yangu ninaamini hata hapa Pangani tunao
wachezaji wazuri kupitia timu zetu hizi zilizoshiriki ligi hii ya Mwidau CUP
ambao wana uwezo wa kufanya vizuri katika timu kubwa za ndani na nje ya nchi yetu,”
alisema Mwidau.
No comments:
Post a Comment