Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
SHIRIKISHO
la Soka nchini (TFF), limesema ili Uwanja uweze kutumiwa katika mechi za Ligi
Kuu unahitajika kuandaliwa vizuri, ikiwa ni pamoja na kuwa na eneo zuri la
kuchezea, uzio na maeneo ya kukaa kwa mashabiki na wahusika wengine.
Maneno ya
TFF yanaweza kuwa majibu kwa Wilaya ya Handeni inayojipanga kuhakikisha uwanja
wao wa Azimio uliyopo wilayani humo unaweza kutumiwa katika mechi za ligi kuu,
kwa kupitia timu ya Mgambo Shooting yenye maskani yake Kabuku wilayani Handeni.
Akizungumza
mwishoni mwa wiki iliyopita, Msemaji wa TFF, Boniface Wambura, alisema kwamba
kuwa na timu inayoshiriki ligi kuu ni jambo moja na uwanja uliopo kwenye timu
hiyo kutumika ni jambo jingine, hivyo ni wakati wa kuukarabati uwanja huo.
“Hata kama
si uwanja huo kutumiwa kwenye ligi kuu, bado unaweza kuingizwa kwenye programu
ya ligi daraja la kwanza na mashindano mengine, lakini hadi uwe kwenye
mazingira mazuri.
“Uwanja
wowote lazima uwe katika kiwango kizuri kama vile sehemu ya kuchezeaa, vyoo,
uzio, majukwaa na mengineyo ya msingi, hivyo kama baadhi yake kwenye uwanja huo
hakuna ni jukumu la kuweka mipango kuuweka sawa,” alisema Wambura.
Katikati
ya mwezi Desemba, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Handeni, Thomas Mzinga,
alizungumzia hamu ya kuona uwanja wao unatumiwa katika mechi mbalimbali zenye
ushindani, zikiwapo timu za Simba na Yanga.
No comments:
Post a Comment