Na Mwandishi Wetu, Kilindi
WAENDESHA Boda Boda wilayani
Kilindi mkoani Tanga wameiomba Mamlaka ya Mapato mkoani Tanga (TRA), kuwapeleka
wilayani humo huduma ya upatikanaji wa leseni kutokana na vijana wengine
kutokuwa nazo hali inayochangiwa na kutokwepo kwa ofisi inayoshughulika na
masuala hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, DC Selemani Liwowa, pichani.Kilio hicho kilitolewa hivi karibuni na wananchi wa kata ya Kwediboma wilayani hapa wakati wakizungumza ambapo walisema kwa muda mrefu wamekuwa wakiikosa kitendo ambacho kinawalazimu kusafiri mpaka Tanga mjini ili kufuata huduma hiyo.
Evarist Mosha mkazi wa kata
hiyo na dereva wa bodaboda alisema kukosekana kwa huduma hiyo wilayani humo
serikali inakosa mapato kutokana na waendesha boda boda wengi kutokuwa na leseni.
Akizungumzia suala hilo, Mkuu wa wilaya ya
Kilindi, Suleiman Liwowa alisema ni kweli katika wilaya hiyo hakuna ofisi za
mamlaka ya mapato (TRA) na kutaka uwekwe utaratibu ambao utawafikia wananchi na
endapo watakubaliana nao wataweka mazingira mazuri ya upatikaji ofisi.
No comments:
Post a Comment