Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KLABU ya Coastal Union ‘Wagosi wa Kaya’, kurejea nchini leo
saa kumi alasiri kutoka Muscat, Oman kwa ndege ya shirika la Oman Air.
Taarifa ya Mwenyekiti wa Coastal Union Hemed Hilal
‘Aurora’iliyotumwa katika vyombo vya habari inasema timu yao ikiwa nchini Oman
imepata mafunzo na mapumziko mazuri kutokana na ratiba nzuri iliyopangwa na
kocha wao Yusuf Chipo.
Alisema kuwa Wagosi wa Kaya walikuwa Oman kwa wiki mbili
sasa, waliwasili nchini humo Alhamisi ya Januari 9 mwaka huu, huku wakirejea
leo Alhamisi ya Januari 23, kwa ajili ya kuanza mbio za Ligi ya Vodacom, ambapo
mzunguuko wa pili utaanza Jumamosi.
“Nashukuru malengo
yetu yametimia, sitaki kuahidi mengi lakini naamini wapenzi wa Coastal Union,
watajionea wenyewe matunda ya kambi hii ya wiki mbili.
Wagosi, wanaoshika nafasi ya nane katika ligi kuu walicheza
mechi ya awali dhidi ya Al Mussannah Club inayoshika nafasi ya saba katika ligi
kuu ya hapa, Wagosi wakatoka na ushindi wa mabao 2-0. Mechi ya pili walicheza
na timu iliyo daraja la kwanza iitwayo Oman Club, nao waliambulia kibano cha
mabao 2-0 kutoka kwa Wagosi wa Kaya,” alisema.
Mechi ya tatu Wagosi walikumbana na kisiki cha Fanja Club
inayoshika nafasi ya tano katika ligi ya Oman, ambapo coastal Union walipokea
kichapo cha bao moja kwa ubuyu. Katika mechi ya nne nay a mwisho Coastal Union,
ilitoa suluhu ya bila kufungana na timu ngumu ya Oman inayoshika nafasi ya nne
Mechi ya kwanza mzunguko wa pili Wagosi watacheza na JKT
Oljoro katika uwanja wa mkwakwani Januari 25 siku ya Jumamosi, na siku ya
Jumatano Januari 29 Wagosi watashuka dimbani kumenyana na Yanga ya jijini
katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
No comments:
Post a Comment