CHAMA Cha Mapinduzi CCM wilayani Handeni, mkoani Tanga,
kimepania kuhakikisha kuwa hakuna chama chochote cha upinzani kinachoweza
kutamba katika Uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji utakaofanyika mapema
mwaka huu.
Mwenyekiti wa CCM wilayani Handeni, mkoani Tanga, Athumani Malunda, pichani.
Akizungumza mjini hapa, Mwenyekiti wa CCM wilayani Handeni,
mkoani Tanga, Athuman Malunda, alisema kuwa wamejipanga kama chama kulinda
heshima yao kwa kuongoza katika serikali za mitaa na vijiji.
Alisema kuwa ili watimize adhma yao, wataweka mfumo mzuri wa
kuweka uongozi unaokubalika kwa wananchi wengi badala ya kupitisha mtu ambaye
si chaguo la wananchi wao.
“Tumejipanga kupita kiasi kwa kuhakikisha kuwa chama
kinashinda katika mitaa yote na vijiji vilivyopo katika wilaya ya Handeni
mkoani Tanga, ili pia iwe chachu ya kupatikana uongozi bora katika Uchaguzi
Mkuu mwaka 2015.
“Tukimaliza kupata wenyeviti wetu itakuwa njia nzuri ya
kupata madiwani na mbunge pia, bila kusahau rais ambaye hapana shaka atatoka
katika chama makini chenye dhamira ya kuwapatia maisha bora Watanzania wote,”alisema
Malunda.
Wakazi wengi na wananchi wa Handeni wameendelea kuwa na
imani na chama hicho kikongwe barani Afrika kutokana na kuwathamini katika
chaguzi mbalimbali na kuwachagua wagombea wao kuanzia wenyeviti wa serikali za
mitaa, vijiji, madiwani, mbunge na Rais pia.
No comments:
Post a Comment