Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mkutano wa CCM Mkoa wa Mbeya.
Wakati CCM inatimiza miaka 37 tangia kuanzishwa kwake februari 5 mwaka
1977,Chama hicho kinajivunia sana mafanikio makubwa kiliyopata hasa
katika kudumisha Umoja na Mshikamano kwa Watanzania ,kutunza na
kuilinda Amani ya nchi hii na kujenga misingi imara ya uchumi wa
nchi,akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano CCM
Mkoa wa Mbeya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye alisema sherehe za miaka 37 zimeanza nchi nzima na
zilizinduliwa rasmi tarehe 26 na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar)
Dk.Ali Mohamed Shein Unguja Zanzibar.
Sherehe
hizi zitahitimishwa hapa jijini Mbeya kwenye uwanja wa Sokoine na
zitahitimishwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.
Viongozi
mbali mbali wa Kitaifa wa CCM wameanza kuwasili na kesho anategemewa
kuwasili Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Philip Japhet Mangula
ambaye pia ni mlezi wa mkoa wa Mbeya akitanguliwa na Katibu Mkuu wa CCM
Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana.
Nape alisema “Tarehe 2 asubuhi saa moja kutakuwa na matembezi ya
mshikamano yatakayoongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama ,Rais Jakaya
mrisho Kikwete matembezi hayo yatafanyika kwenye jiji la Mbeya yataanzia
eneo la Soweto na yataishia kwenye ofisi za CCM mkoa wa Mbeya, baada ya
matembezi hayo wananchi watakwenda kwenye viwanja vya Sokoine ambapo
kutakuwa na burudani mbali mbali vikiongozwa na TOT, Vikundi vya muziki
wa kizazi kipya, sherehe hizo zitaonyeshwa moja kwa moja na baadhi ya
televisheni pamoja na kurushwa moja kwa moja na baadhi ya radio.
Wakazi
wa Mbeya waombwa kujitokeza kwa wingi wakati wa mapokezi ya Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi tarehe moja na pia washiriki kwenye matembezi
na sherehe zitakazofanyika tarehe2.
Maadhimisho
ya sherehe hizi yataambatana na shughuli mbali mbali nchi kote ,ikiwa
pamoja na shughuli za utunzaji wa mazingira kama kupanda miti,kushiriki
shughuli za maendeleo kujenga shule na zahanati,usafi pamoja na
kutembelea wagonjwa hospitalini.
No comments:
Post a Comment