Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa mshtuko taarifa za tukio la kutekwa, kuteswa na kuumizwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Temeke, Josephat Yona Patrick.
Chama kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano
na Uhusiano, mbali ya kukemea kwa nguvu zote tukio hilo la kihuni na mengine ya
namna hiyo yenye lengo ya ukatili dhidi ya binadamu, katika hatua ya sasa
kinapenda kusema yafuatayo juu ya tukio hilo ovu ;
namna hiyo yenye lengo ya ukatili dhidi ya binadamu, katika hatua ya sasa
kinapenda kusema yafuatayo juu ya tukio hilo ovu ;
1. Jeshi la
Polisi lifanye uchunguzi juu ya tukio hilo la kutekwa na kuteswa
kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Temeke ili ukweli ujulikane na haki
itendeke, kwa sheria kuchukua mkondo wake.
2. Chama
kinawataka wanachama na Watanzania kwa ujumla kutulia, hasa pale ambapo
watu wenye hila na malengo yao, wanaanza kukihusisha chama na tukio
hilo. Watambue kuwa pamoja na mtu yeyote kuwa kiongozi wa chama, bado
anayo maisha yake na uhusiano na watu wengine katika jamii.
3. Jeshi
la Polisi linapaswa kuyachukulia uzito mkubwa na unaostahili matukio ya
namna hii ambayo yanaanza kuota mizizi kutokana na watu waovu
wanayoyatekeleza kutochukuliwa hatua za kisheria ambazo zingesaidia
kuzuia yasitokee tena.
4. Watanzania
bado wanakumbuka kwamba hadi sasa Jeshi la Polisi limeshindwa kutoa
taarifa za kina na kuchukua hatua za kisheria ambazo zingesaidia ukweli
kujulikana na haki kutendeka katika matukio ya kutekwa na kuteswa kwa
kiongozi wa madaktari Dk. Steven Ulimboka na Mwenyekiti wa Jukwaa la
Wahariri, Absalom Kibanda. Hivyo ingesaidia kuzuia
matukio mengine kutokea.
matukio mengine kutokea.
5. Ni
kutokana na jeshi hilo kushindwa kuwajibika ipasavyo katika matukio
mengine ya namna hiyo, watu waovu wanaweza kutumia mwanya wa
kinachoendelea ndani ya CHADEMA kwa chama kuchukua hatua za kinidhamu
dhidi ya wanachama wasio waadilifu, kufanya matukio ya namna hiyo
ili kujenga taswira ya kukihusisha chama na uhuni huo unaobeba kila sifa
ya kuitwa ukatili dhidi ya binadamu.
6. Aidha
kushindwa kwa Jeshi la Polisi kuwajibika ipasavyo katika kufanya
uchunguzi wa matukio hayo (yaliyotolewa kama mfano hapo juu) na mengine
ya namna hiyo, jeshi hilo linazidi kujiweka katika wakati
mgumu wakukwepa tuhuma za baadhi ya watendaji wake kujua na kushiriki
masuala haya, hususan kwa kurejea tukio la kutekwa kwa Dkt. Ulimboka.
Imetolewa jana Jumanne, Januari 7, 2014 na;
Kurugenzi ya Mawasiliano na Uhusiano
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
No comments:
Post a Comment