Na Rajabu Athumani, Handeni
WATU wanne wamekufa papo hapo na mmoja hospitali katika ajali ya basi
aina Noa ilitokea jana majira ya jioni katika Kitongoji cha Mtakuja
kata ya Misima wilayani Handeni na kujeruhi wengine wawili.
Mmoja wa shuhuda wa ajali hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la
Rashidi alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kukatika kwa chuma
kinajulikanacho kama propera shafti
ambacho kilikatita na kusukuma gari pembeni na kupinduka zaidi ya mara
tatu na kusababisha vifo hivyo na majeruhi.
Habari kutoka eneo
la tukio zilieleza kuwa dereva wa gari hilo aliyejulikana kama Miraji
Shabani(22) ametoroka baada ya ajali kutokea na hajulikani alipo hadi
sasa na polisi wanaendelea kumtafuta kwa mahojianao.
Kamanda wa
polisi mkoa wa Tanga Costantine Massawe alithibitisha kutokea kwa ajali
hiyo na kusema kuwa ni kweli gari yenye namba za usajili T493 AUH aina
ya Noa na kuua watu wanne hapo hapo na mmoja hospitali baada ya kukatika
chuma wanachoita propera shafti hali iliyosababisha kuuwa watu watano
katika ya saba waliokuwa katika Noa hiyo.
Kamanda Massawe
alisema kuwa Noa hiyo ilikuwa ikitokea Handeni mjini kuelekea Misma
kilomita 16 kutoka mjini ikiwa na wanafamilia hao saba wakiwa humo
kwaajili ya shughuli zao binafsi za kifamilia na haikuwa gari ya
kibiashara.
Kamanda Massawe aliwataja marehemu wa ajali hiyo
kuwa ni Juma Nyeri (90) mkazi wa Misima,Athumani Yusuph (45),Zahara
Changogo,Mwajuma Mzimu na Zuberi Abdallah wote wakazi wa Suwa wilayani
Handeni na majeruhi ni Hemedi Said ambae baada ya kupatiwa matibabu
alipewa ruhusa na kurudi nyumbani pamoja na dereva ambae alishakimbia
hiyo haijulikani kuwa ameumia kiasi gani..
No comments:
Post a Comment