Na
Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BENDI
ya muziki wa dansi hapa nchini ya Skylight, usiku wa kuamkia leo, ilifanya
shoo ya aina yake katika maadhimisho ya miaka 20 ya Club Bilicanas,
iliyofanyika katika ukumbi huo wenye hadhi ya Kimataifa.
Skylight
iliweza kutoa burudani kabambe kwa mashabiki na wadau wa burudani walioingia
kwa wingi katika ukumbi huo unaopendwa na wengi hapa nchini kutokana na
mazingira yake.
Sehemu ya wanamuziki wa bendi ya Skylight wakiwa kazini
Akizungumzia
maadhimisho hayo, mkurugenzi wa Club Bilicanas, Frank Charles, alisema sherehe
hizo ni kufurahia uwepo wao kwenye burudani kwa miaka 20 tangu kuanzishwa
kwake, huku wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya, maarufu kama Bongo
Fleva, wakipangwa kuonyesha uwezo wao jukwaani.
Mbali
na Club Bilicanas kusherehekea miaka 20 ya burudani nchini, pia Kampuni ya
Clouds Media Group, nayo ilisherehekea miaka 13 ya kazi yao, katika ukumbi huo, ikiwa ni baada ya
kufanya maandalizi kwa kushirikiana.
Hata
hivyo, burudani hizo nusura ziharibike baada ya mvua kuanza kuzengea katika
maeneo hayo, hivyo wadau waliokuwapo ndani ya uzio ambao shughuli ilikuwa
ikifanyika, walikimbilia ndani.
Viingilio
katika sherehe hizo zimepangwa kuwa Shilingi 10,000
na kwa wale waliolipa sh 15,000 walipata fursa ya kujumuika katika burudani nje
na ndani ya ukumbi na pia kulipoandaliwa kwa ajili ya burudani hizo.
Wasanii
waliopangwa kufanya burudani kwa pamoja walikuwa ni Skylight bendi, Ommy
Dimpoz, Linah, Recho, Amini, Richie Mavoko, Barnaba, Makomandoo na Bob Junior,
maarufu kama Rais wa Masharobaro.
Club
Bilicanas ilianza rasmi kutoa burudani mwaka 1992 na ndani ya muda wote huo
imejikusanyia sifa na wateja lukuki wa ndani na nje ya nchi kutokana na
programu mbalimbali zinazondeshwa ndani ya Club hiyo.
No comments:
Post a Comment