Unafanyaje kumpa raha mwenzako?
Wawili wapendanao wakiwa wanajiachia kwa raha zao
Na Kambi Mbwana, Handeni
MAPENZI ni jambo ambalo linaleta hisia mbili tofauti. Mosi;
mapenzi yanaweza kukufanya uishi kwa raha kama
mfalme. Pili, mapenzi hayo yakibadilika hukufanya uwe kama
chizi.
Jambo hilo zuri
linalofananishwa na sukari kwa yaliyowakalia vizuri, hubadilika na kuwafanya
baadhi yao
waone ugumu wa kuendelea kuishi, maana wanaowapenda wanawasumbua kwa kiasi
kikubwa.
Ni kutokana na hilo, jamii
inashauriwa kuwa makini katika suala hilo.
Wasijaribu kukurupuka na kuchukua uamuzi wenye mashaka kwa namna moja ama
nyingine, maana vinginevyo watatamani kujinyonga.
Hata hivyo, pamoja na yote hayo, lakini inajulikana wazi
wazi kuwa dawa kubwa katika uhusiano wa kimapenzi ni kumfikisha mwenzako,
kumuweka katika kilele cha ubora katika ulimwengu wa mapenzi.
Katu usiangalie umbo lako, sura yako katika kujigamba kwamba
unaweza kupendwa na yoyote, wakati ni mzigo kitandani. Kama
huna ujuzi katika suala la mapenzi, ondoa kupendwa, kuhitajiwa au kugandwa na
yoyote.
Zaidi ya hapo, wachache wao watakupitia na kuchukua hamsini
zao, maana huna ujanja wa kumuweka mwenzako katika furaha. Hivyo basi, ili
jamii iwe kwenye ramani nzuri na furaha ya mapenzi, lazima tuwajulie watu wetu.
Tufahamu namna ya kuwachanganya kisaikolojia, bila kuangalia
uzuri wetu, fedha zetu, maana hizo haziwezi kufanya penzi liwe na amani.
Wapo ambao wanaishi na wanaume wenye nazo kupita kiasi,
lakini bado wake zao, wachumba zao au wapenzi wao wanajiingiza katika uhusiano
na watu wa kawaida, wakiwamo wafanyakazi wa ndani.
Hata hivyo haitoshi, wapo pia wakina mama wenye nazo lakini
wanachanganywa na wasichana wa kawaida, wenye sura za kawaida au hadhi za
kawaida. Wenye mali
zao wanalia na kusaga meno.
Wanasema“Hivi kwani mume wangu unatembea na yule mfanyakazi
wa ndani wakati mimi nipo” Au sielewi unachofuata kwa yule kijana mchunga mbuzi
wakati mimi nipo, tena mwenye fedha za kutosha tu”
Kama wewe ni miongoni mwa
watu wenye mtazamo huo umeliwa. Fedha sio kila kitu katika mapenzi. Fedha zako
usipoangalia zinaweza kuwanufaisha wapita njia, wajuzi wa mambo kwenye mambo
fulani muhimu.
Huo ndio ukweli wa mambo. Mjuzi huyo hatafutwi ili mradi mtu
ana mtu wa nje, ila umuhimu wake unakuja anapokuwa kwenye ulingo. Hayo lazima
mimi na wewe tuyajuwe kwa ajili ya mapenzi yetu.
Unapokuwa na mpenzi wako, mume au mke wako lazima ujuwe yupo
na wewe kwa ajili ya kujenga maisha ya wawili. Ili mwenzako afurahie uwepo
wako, hakikisha kuwa walau unatumia muda wako hata kama
kidogo kumridisha kimapenzi.
Kwa wale ambao kwa miaka mingi wameishi na wapenzi wao bila
kutumia ujuzi wao, waanze leo. Na wale wanaoingia kwenye uhusiano leo, pia
wawaangalie watu wao, namna gani walivyo na wanastahili aina gani ya mapenzi.
Ninaposema mapenzi, sio yale ya kukaa pamoja, kutembea
pamoja au kumpigia simu kila baada ya dakika kumi. Mapenzi, tendo la ndoa lenye
ujazo mkubwa linalostawisha uhusiano wa wawili wapendanao.
Hivyo basi tuwe makini katika kazi hiyo. Tukitaka kuwapa
raha kweli wenzetu lazima tuache kazi na kufanya kazi. Tendo la ndoa sio mchezo
mdogo. Sio kama kuwasha njiti ya kibiriti mahala palipotulia.
Inahitaji kusumbua akili na kusumbua pia mwili wako. Sina
maana kama nataka muda wote muwe kwenye tendo
la ndoa, ila mnapotaka kufunja amri hiyo ya sita, basi mfikishe mwenzako
kileleni.
Usimchezee chezee tu ukamuacha. Nimeamua kuandika mada haya
maana nimepata malalamiko mengi kutoka kwa wanawake. Baadhi ya wasomaji wangu,
wamenipasha kwamba waume zao ni watu wa kwenda raundi moja halafu wanaangalia
ukutani.
Kwa bahati mbaya, watu hao wanapolala uzungu wa nne,
wanakuwa wanawanyanyasa wenzao, kama unavyojua
tena gari linapowaka. Hali hiyo inakera kiasi cha kutamani wapiti njia.
Haya nayasema kwa uchungu, maana usaliti mwingi huibuka kama wawili wapendanao hawaridhishani. Kama
unaona huna ujuzi wa kumuweka katika kilele mwenzako, tafuta msaada kwa watu.
Kabla ya kuendelea, niseme tu kutokana na aina ya gazeti
lako la Mtanzania, tunashindwa kuandika kiundani zaidi mada za mapenzi, badala
yake tunakuwa wepesi kujibu maswali yenu kwa kupitia simu au barua pepe.
Tunafanya hivyo baada ya kugundua kwamba watoto wengi nao
hujifunza kinachoandikwa kwenye gazeti, jambo linalonifanya niandike kwa
kuficha au yale yasiyokuwa ya ndani zaidi.
0712 053949
0753 806087
No comments:
Post a Comment