MSIMU wa kumi na moja wa mbio za kimataifa za
Kilimanjaro Marathon zinazotarajiwa kufanyika Machi 3, mwaka 2013, umezinduliwa
mjini hapa juzi, katika Ukumbi wa Morio Hall, ikiwa ni dalili kuwa patashika
hizo zitaanza katika Mkoa wa Kilimanjaro.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Leonidas Gama, wa pili kutoka kulia, akishuudia uzinduzi wa mashindano ya Kilimanjaro Marathon, yaliyozinduliwa jana, mkoani humo.
Akizungumza katika uzinduzi huo Meneja wa Bia ya
Kilimanjaro Premium Lager ambayo ndiyo wadhamini wa mashindano hayo, George
Kavishe, alisema wamedhamiria kufanya mabadiliko makubwa katika mbio hizo ili
kuziendesha Kimataifa zaidi.
“Sisi kama wadhamini wakuu wa mbio hizi
zinazoshirikisha wakimbiaji kutoka kila kona ya Dunia, tumedhamiria kuhakikisha
tunaboresha mbio hizi na kuzifanya kuwa sura ya kimataifa,” alisema Kavishe
Alisema kutokana na matokeo ya mbio za mwaka
huu, yaliyofanyika mapema Februari, na kushuhudia wakenya wakitawala mbio hizo,
safari hii wamejipanga kwa kutoa changamoto ya zawadi zaidi ya kawaida kwa
washindi.
“Tumeboresha mashindano nah ii ni kitu kipya ,
kwani kutokan ana aibu ya mashindano ya mwaka huu, mwaka ujao kila mshindi wa
kwanza kutoka ndani ya nchi atapata maara mbili ya fedha za mshindi wa kwanza,”
alisema Kavishe.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,
Leonidas Gama katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya ya
Moshi, Dkt.Ibrahimu Msengi, aliwataka wanariadha wote watakaoshiriki
kuhakikisha kuwa kile kilichotokea katika mashindano ya liyopita hasa ya mwaka
huu yanbaki kuwa sehemu ya historia.
Alisema Mkoa umefurahishwa sana kuwepo kwa mashindano hayo mkoani hapa
na antarajia mbio hizo zitachangia katika kukuza sekta ya Utalii, Uchumi na
mahusiano ya kimataifa kutokana na kushirikisha wakimbiaji kutoka mataifa
mbalimbali kutoka katika kila kona ya dunia.
Wakati huohuo Mwenyekiti wa chama cha Riadha
mkoani Kilimanjaro (KAA), Liston Nepacha alibainisha kuwa kwa kushirikiana na
chama cha Riadha Taifa (RT), wamedhamiria kufuta mapungufu yote yaliyojitokeza
katika mbio za mwaka huu na kuongeza kuwa tayari ya kikosi cha Tanzania
kinaendelea na Maandalizi katika Kambi yao iliyopo Holili, Himo mkoani Hapa.
Mashindano ya Kilimanjaro Marathon yanayofanyika
kila Mwaka yanadhaminiwa na Kilimanjaro premium Lager, Kilimanjaro Drinking
Water, Arusha Hotel, Gapco wanaodhamini mbio za watu wenye Ulemavu, Bonite,
Kiss Hotel, TPC, Shoprite, KK security, Simba Cement, Merenga Investment, CFAO
Motors na yanatarajia kuwa na washiriki wapatao 6000.
No comments:
Post a Comment