Na Kambi Mbwana, Handeni
LICHA ya Serikali kwa kupitia Mkuu wa Wilaya ya Handeni,
Muhingo Rweyemamu, kupiga marufuku wafugaji kupitisha ng’ombe zao katika
barabara inayoendelea na ujenzi wake, kuanzia wilayani Korogwe hadi Handeni,
amri hiyo inavunjwa kutokana na mifugo kupitishwa, hivyo kuiharibu kabla
haijakamilika.
Uchunguzi uliofanywa na Handeni Kwetu na kuweka ushahidi wa
ng’ombe kunaswa na kamera yetu, ulibaini jinsi amri hiyo inavyovunjwa na
wafugaji pamoja na wenyeviti wa vijiji vinavyopita katika maeneo yao kushindwa
kuwadhibiti.
Wakizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina yao, wakazi wa
kijiji cha Komsala, walisema kuwa uongozi wa kijiji chao hauna nguvu ya
kuwazuia wafugaji hao wanaopita mara kwa mara kwenye barabara mpya.
Hao ndio njia yao, maana hawa wafugaji wanapenda kupitisha
katika barabara mpya na hakuna wa kuweza kuwazuia, wakiwapo viongozi wa kijiji
chetu na wote.
Hii barabara itaharibika kabala haijakabidhiwa au
kuchelewesha kukamilika kwake, maana wenzetu ni wazito kuelewa na wengineo
wanalingia fimbo zao,” waliiambia Handeni Kwetu mapema leo, baada ya makundi ya
ng’ombe kuonekana zikipita barabara mpya na kuacha ya zamani.
No comments:
Post a Comment