https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Sunday, March 30, 2014

Simba yachapwa 2-1 na Azam, huku Yanga nayo ikipigwa bao 2-1 na Mgambo Shooting jijini TangaTimu ya Azam FC, leo imefanikiwa kuifunga bao 2-1 timu ya Simba, iliyojitoa kabisa katika mbio za ubingwa na kuziacha Yanga na Azam wakipumuliana kuwania taji hilo la Tanzania Bara.

Mabao ya Azam yalifungwa dakika ya 15 kupitia kwa Khamis Mcha na John Bocco dakika ya 56, wakati bao la Simba la kufutia machozi lilipatikana dakika ya 45 kupitia kwa Joseph Owino.

Katika mechi iliyopigwa katika Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, Yanga walishindwa kufurukuta baada ya kukubali kichapo cha bao 2-1 kutoka kwa timu ya Mgambo Shooting, yenye maskani yake Kabuku, wilayani Handeni, mkoani Tanga.

 

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...