https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Saturday, March 01, 2014

Kaseba: Mashali hana uwezo wa kupambana na mimiNa Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BONDIA wa ngumi za kulipwa hapa nchini, Japhet Kaseba, amesema kwamba mpinzani wake Thomas Mashali hana uwezo wa kupambana nay eye Machi 29, pambano litakalopigwa katika Ukumbi wa PTA Sabasaba.
Japhet Kaseba, pichani
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kaseba alisema kuwa amekuwa na uchu wa kutoa kichapo kupita kiasi, hivyo haamini kama anaweza kupigwa na bondia mwingine yoyote.

Alisema kuwa kikubwa kinachompa imani ya kumchakaza Mashali ni umahiri wake wa kurusha masumbwi, jambo linalomfanya ajione yupo juu kimasumbwi.

“Najiandaa vizuri kuhakikisha kuwa umahiri wangu haufutwi na bondia mwingine yoyote, akiwamo Mashali ambaye nakutana naye nikiwa na hasira kupita kiasi.

“Naamini hawezi kuninyamazisha kwakuwa nimejipanga na hakuna jingine zaidi ya kujiandaa vyema ili nijiweke katika mazingira mazuri,” alisema.

Kaseba ni miongoni mwa mabondia wenye makali ya kutisha katika tasnia ya masumbwi nchini, huku pia akiwahi kuwa Bingwa wa Dunia wa ngumi na mateke.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...