Twanga Pepeta kuiacha Dar kwa wiki moja, kutembelea pia Mbamba Bay mkoani Ruvuma
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BENDI ya The African
Stars, Twanga Pepeta, itakuwa nje ya jiji la Dar es Salaam kwa wiki moja,
kutokana na kuwa na ziara ya kuinadi albamu yao ya Nyumbani ni Nyumbani, katika
mikoa ya Njombe, Ruvuma na Mbeya kuanzia Machi 26 mwaka huu.
Kiongozi wa bendi ya Twanga Pepeta, Luiza Mbutu, akifanya mambo jukwaani katika moja ya maonyesho ya bendi yake.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa bendi hiyo, Hassan Rehani, alisema kuwa Machi 26
wataanza na shoo katika Ukumbi wa Turbo Hall, uliopo mkoani Njombe, wakati siku
inayofuata watacheza na mashabiki wao Mbamba Bay, katika Ukumbi wa Bay live
Social Hall.
Mwimbaji wa Twanga Pepeta, Kalala Junior, katikati akionyesha umahiri wake wa kucheza na jukwaa katika moja ya maonyesho ya bendi yake.
Alisema Machi 28 bendi
yao itafanya shoo katika Ukumbi wa Serengeti, uliopo mjini Songea, wakati Machi
29 Twanga watatumbuiza City Pub, mjini Mbeya, huku Machi 30, wakifanya shoo
High Class, uliopo mjini Tunduma.
“Hizi ni ziara maalum
kwa ajili ya kwenda kuinadi albamu yetu na bendi yetu kwa ujumla, hivyo naamini
wadau tutakuwa nao bega kwa bega.
“Tunaomba tushirikiane
kwa nguvu mashabiki wetu ambao kwa kiasi kikubwa tumeamua kuwapelekea bendi yao
ili wafurahie burudani za Twanga Pepeta,” alisema.
Kwa kuwa na ziara ya
mikoani, sasa wapenzi wa bendi hiyo watalazimika kusubiri kwa siki moja kabla
ya kuanza tena kuipata burudani ya Twanga Pepeta.
No comments:
Post a Comment