Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TIMU ya Coastal Union, yenye maskani
yake jijini Tanga, inajiandaa vizuri kukabiliana na joto katika mchezo wao
dhidi ya Azam utakaopigwa Jumamosi ya Machi 15, katika Uwanja wa Azam Complex,
Chamazi.
Mechi hiyo inachezwa huku kukiwa na
marekebisho kadhaa, hasa kati ya Simba na Costal, waliopangwa kucheza Jumatano,
kabla ya mechi hiyo kusogezwa mbele hadi Machi 23.
Akizungumza jana jijini Dar es
Salaam, Msemaji wa Costal Union, Hafidh Kido, alisema kuwa wanajiandaa vyema
ili kusaka ushindi dhidi ya Azam.
Alisema ingawa wamepata matokeo
mabaya ya sare dhidi ya Ashanti United, ila bado hawajakata tamaa katika
patashika ya Ligi ya Tanzania Bara.
“Coastal bado hatujakatishwa tamaa
katika harakati za kuiweka juu zaidi timu yetu, hivyo kwa sasa tunajiandaa
kuwakabiri Azam.
“Naamini utakuwa ni mchezo mgumu
kupita kiasi, ukizingatia kuwa Azam wao wanasaka ubingwa, hivyo watataka
mbeleko kutoka kwetu, jambo ambalo haliwezekani kirahisi,” alisema.
Simba inayonolewa na kocha wake Zdravko
Logarusic, imeshindwa kuonyesha cheche za kuunyaka ubingwa wa Tanzania Bara,
baada ya kuendelea kupata matokeo mabaya katika mechi zake.
No comments:
Post a Comment