Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu nchini
(TFF), limesema kwamba limejipanga kumpata kocha wa timu ya Taifa, Taifa Stars,
ili aanze mikakati ya kuinoa timu hiyo.
Stars imerejea nyumbani huku
ikishindwa kuwatambia wenyeji wao Namibia, baada ya kutoka sare ya bao 1-1,
katika mechi ya Kimataifa ya kirafiki.
Akizungumza jana jijini Dar es
Salaam, Msemaji wa TFF, Boniface Wambura, alisema kuwa mchakato huo wa kumasaka
kocha mpya wa Stars umeshaanza, wakiwa na imani ya kumpata haraka iwezekanavyo.
Alisema kocha Salum Madadi alikuwa
wa muda kwasababu ana majukumu mengine ya kiutendaji ndani ya TFF, hivyo
wanaamini hilo litafanikiwa.
“Tunahitaji kuwa na kocha bora na
timu yenye nguvu zaidi, hivyo naamini kinachofanyika sasa ni kupigania
uwezekano wa kupatikana mbadala wa Madadi.
Hata mipango ya kuiendeleza na
kuiandaa zaidi timu yetu ya Taifa itafanikiwa endapo benchi la ufundi
litasimama imara baada ya kukamilisha mchakato wa upatikanaji wake,” alisema
Wambura.
Ajira ya kocha wa Stars, Kim Poulsen
ilifikia ukingoni, hivyo kulazimika TFF kumteua Madadi kukaimu nafasi yake kwa
ajili ya mechi dhidi ya Namibia.
No comments:
Post a Comment