Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
DIWANI wa Mondo, wilayani Kondoa,
mkoani Dodoma, Said Sambala, amesema vijana wengi wa kata yake wana vipaji
imara vya kucheza soka, hivyo juhudi zinahitajika kuwaendeleza.
Akizungumza jana jijini Dar es
Salaam, Sambala alisema vipaji hivyo vilionekana katika mashindano ya Kombe la Diwani,
yaliyoandaliwa na yeye ili kuendeleza soka la kata yake ya Mondo.
Alisema anaamini juhudi za
kuendeleza vipaji vya soka kwa vijana wake wa Kata ya Mondo zitafanikisha kwa
kiasi kikubwa kuwapatia mwangaza vijana hao na hatimaye kufanikiwa kuonesha
cheche zao.
“Tumegundua Mondo kuna vipaji vingi,
hivyo lazima tuweke mikakati kabambe ya kufanikisha jambo hili, hasa kwa
kusimamia mashindano makubwa yenye nguvu na mguso wa aina yake.
“Naamini mpango huu utakuwa na tija
kwa kiasi kikubwa, ukizingatia kuwa katika mashindano ya diwani Cup mwaka jana,
watoto wengi tuliwashuhudia wakifanya mambo mazuri uwanjani,” alisema.
No comments:
Post a Comment