Hivi
karibuni watakutanishwa miamba miwili ulingoni wote wakiwa na nywele
zilizotengenezwa kwa mtindo wa rasta,
Miamba hiyo ambayo mara nyingi huwa ndio gumzo la watu
mitaani hususani wapenda mchezo wa ngumi kwa tabia zao na vibwekwa vyao kwa raia wa kawaida, hao si wengine bali ni
Japhet Kaseba na bondia mtukutu Thomas Mashali, pichani, Jumamosi ya Machi 29 katika Ukumbi PTA, Sabasaba.
Kwa Mfano -
bondia Thomas mashali “samba asiyefugika
– kama anavojiita” alizaliwa Sept 1989 na kukulia mitaa ya manzese jijini dare
s salaam,akiwa mtoto mtundu,mkorofi,mgomvimgovi na mpenda michezo kama ilivyo kwa mdogo wake
Charles mashali ambaye na yeye pia alikuwa
bondia mzuri aliyetokea kuwashinda na kuwasumbua mabondia wengi kama kina Francis Miyeyusho na alishawahi kuchukua Ubingwa wa Taifa kabla ya kuachana na mchezo
wa ngumi kwa kuumia bega.
Alishindwa kuendelea na mchezo wa
ngumi na kumuachia Thomas mashali ambae ni mkubwa kwa Charles mashali aliyeanza
mchezo wa ngumi akiwa mdogo na kupigana
mapambano katika kumbi za colin na
manyala park za manzese na hapo udogoni
amewahi kucheza na kina Ramadhan miyeuyusho,
Raston Phili ‘moto wa tipa’ na marehemu papa upanga na kuwa kivutio cha wengi
ulingoni na kero kwa wengine uraiani kwa
tabia yake ya kuwapigapiga watu na kuwaonea
wasio na hatia na kuendekeza ubabe usio na maana akiwa kama tembo wa mitaa ya manzese
kwa tabia yake hiyo kulimfanya awe
anakwenda jela mara kwa mara na
kumpotezea dira imara katika masumbwi na
kukaa muda mrefu bila kupigana mpaka pale kuna wakati ametoka jela na kurudi
tena gym kama ilivyo kawaida yake kiasili anapenda sana mazoezi na michezo
alikuwa akijifua kuuweka mwili wake fiti.
Mwaka 2009 alipotokea jamaa mmoja
anayeitwa juma shumbili ambae ni promota wa mapambano madogomadogo ya mchangani
lakini kwa wakati huu alikuwa anaandaa zaidi katika ukumbi wa texas hall manzese
na kumuandalia pambano Thomas mashali akiwa kama mbabe wa Manzese na Amadu Mwalimu akiwa kama mbabe wa Tandika.
Matokeo yake Mashali aliibuka
mshindi wa pambano hilo kwa kumpiga Mwalimu kwa nokauti ya raundi ya tatu na hili ndilo pambano lake la
kwanza rasmi la kulipwa na kumuingiza
katika rekodi ya mabondia wa kulipwa
nchini na kumfanya watu wahamasike zaidi kutaka kumuona katika mapambano
mengine akikutana na wababe wenzake.
Hatimaye alikutana na Yasin Abdallah ‘ustadh’ Rais wa Oganaizesheni wa Ngumi za kulipwa Tanzania na kumsihi Mashali aachane na mambo ya kihuni atulie katika mchezo wa ngumi,
kwani ana kipaji nao.
Ustadh
alijitahidi kumtafutia mapromota na
kucheza mapambano mbalimbali na mabondia wakali na kuwashinda, hatimae april
2012 alikutanishwa na seleman galile kugombania ubingwa wa taifa wa TPBO ambao
alishinda mchezo huo kwa point na kuuchukua ubingwa huo tabu sana katika
pambano gumu,ubingwa ambao bado
anaushikilia mpaka hii leo.
Na baadae alipata mapambano ya kimataifa na
kuwashinda mabondia wengi wa nje hususani Kenya na Uganda na kutwaa ubingwa wa
Africa mashariki na kati kwa kumchapa medy sebyala wauganda, akiendeleza wimbi
lake la ushindi Thomas mashali “mzee wa ghetto au simba asiye fugika – kama
anavyojiita” viongozi na wadau wa ngumi wakamkubali
na kumuona ameivaa kimchezo wa ngumi, wakaona huu ni muda muafaka wa mashali
kumvaa Francis cheka akiwa kama challenger anayeutaka ubingwa wa cheka, mwaka
may 2013 akapoteza mchezo huo dhidi ya cheka ambao uliokuwa mkali sana kwa
kukata upepo raundi ya nane na kupigwa mwishoni wa raundi ya kumi,mashali
alionesha upinzani mkali kwa cheka, akiwa anajiuliza kapigwaje na cheka alipata bahati nyingine ya kukutanishwa na
bondia wa hapa nchini Mada Maugo na kugombania ubingwa wa Afika wa WBFed (world
boxing federation) na kuibuka kidedea baada ya kumpiga Mada Maugo kwa point, na
kutwaa ubingwa huo afrika akachaguliwa kwenda urusi kugombania ubingwa wa
mabara dhidi ya arif magomedov huko
alipata kipigo kikali toka kwa bondia huyo wa urusi katika raundi za
mwazomwanzo na kurudi nchini mikono
mitupu.
Mashali kwa
Kupoteza mchezo wake na mrusi
hakujaathiri ubingwa wake wa afrika
jambo ambalo viongozi wa ngumi wakiongozwa na Ibrahim kamwe walikaa na
mapromota wakaonelea huyu bwana anaweza
kuzipiga na bondia wa mbeya Karama nyilawila ambao walishawahi kuzipiga zamani
mwaka 2009 na pambano kutolewa sare,
wakati linapangwa pambano hilo la karama na mashali la marudiano, tayari kampuni ya bigright promotion ilishaanza
maongezi ya kuwapiganisha mabondia karama nyilawila na jafet kaseba, akajitokeza
promota maarufu wa jijini Tanga Ally
mwanzoa na kuwa yupo tayari
kuwapambanisha mabondia hao wote katika mapambano ya ubingwa .hapo ndio
mwakilishi wa UBO(universal boxing organization) nchini bw emmanuel mlundwa ambae
pia ni rahisi wa PST( pugilistics syndicates of Tanzania) akasema mashali ana
nafasi ya kupigana Japhet kaseba katika ubingwa huo ulio wazi katika uzani wa kilogram
79.mipango ya pambano hilo ikaanza kwa kuwakutanisha Thomas mashali na
Japhet Kaseba aliyezaliwa Decemba 1979 (miaka 10 zaid ya mashali) ambae ni Bingwa asiyepingika hapa nchini kwa
kukosa bondia wakupigana nae baada ya kuwapiga mabondia wote katika mchezo wa mateke (kickboxing) ambae pia
amewahi kuwa bingwa wa Dunia katika mchezo
huo wa ngumi na mateke (kickboxing)
kwa kushinda ubingwa wa mabara nchini Holand na kuutetea nchini Japan,
na baadae kugombea ubingwa huo wa Dunia dhidi ya bondia toka Ufilipino Ricky
Agayas na kumpiga kwa ko ya raundi ya tatu na kutwaa ubingwa huo. Kaseba amekaa
kwa muda bila kupata nafasi ya kuutetea ubingwa wake huo kwa kukosa wadhamini
na hapo alipoamua kubadili aina ya mapigano na kurudi katika ngumi mchezo ambao
aliucheza zamani kabla ya kickboxing.
Alipoingia tena katika ngumi alipata
nafasi ya kupigana na bingwa wa ngumi wa hapa francis cheka katika pambano la
kuwakutanisha bingwa wa mateke na bingwa wa ngumi matokeo yake kaseba
alishindwa na cheka na kutoridhika na matokeo hayo kwa kisingizio cha fujo
zilizotokea katika mchezo huo na akawa anatafuta marudiano kwa hali yoyote ile na
kumfanya abakie katika ngumi akisubiri nafasi nyingine ya marudiano na cheka akapigana mapambano yake ya ngumi kwa
kusuasua na kufanikiwa kuchukua ubingwa wa taifa wa PST kwa kumpiga maneno osward ubingwa ambao anaoushukilia mpaka leo.
Kaseba
alicheza nchi Australia akigombea ubingwa nchini humo na kupoteza. Katika pambano lililoandaliwa
hivi karibuni kati ya wababe waliopoteza
ughaibuni, ikiwa na maana Japhet kapigwa Ausralia na mashali kapigwa rusia pindi
japhet alijisafisha kidogo kwa kucheza na Alibaba Ramadhan wa Arusha na kumpiga
kwa tabu, jambo ambalo linampa imani Mashali huwenda akamshinda Kaseba.
Marasta hao
ni Japhet kaseba na Thomas Mashali ambao wanaotegemea
upanda
ulingoni tarehe 29 March 2014 katika Ukumbi wa PTA Hall kugombania ubingwa ulio wazi wa Universal Boxing Organization-UBO na mshindi katika
pambano hilo atacheza na Karama Nyilawila Mei Mosi. Limeingia katika sura mpya
ya wadau wengi wa ngumi kuwekeana pesa
kama kamari ya kuwa nani atashinda, tayari amejitokeza msanii Dotnata (ambae ni
mshabiki mkubwa wa Kaseba) kaahidi kutoa gari endapo Kaseba atashinda. Pia kuna
mdau mwingine ameahidi kutoa pikipiki kwa mshindi kati ya Kaseba na mashali siku hiyo katika ukumbi wa Karume zamani PTA hall sabasaba
ambapo kutakuwepo na mapambano mengi ya utangulizi yakiwemo pia ya ubingwa
wakati katika pambano la raundi kumi Fredy Sayuni wa keko atazipiga na Rajabu Mahoja wa Tanga ubingwa wa Taifa, Alan Kamote wa Tanga bingwa wa Afrika Light Weght aliyekuwa azipige na Fadhili Awadh (aliyefariki ghafla kwa maleria) katika pambano la Ubingwa la UBO International sasa atazipiga na bingwa wa taifa katika uzani huo bondia toka
Tanga Said Mundi, nae Juma Fundi atazipiga na mkongwe Haji Juma huku Dogo
anayechipukia kwa kasi Issa Omari Nampepeche wa Dar es Salaam, akizipiga na bingwa wa
taifa bantam Zuberi Kitandula toka Kilimanjaro pia kutakuwepo na pambano la
mabondia wakongwe wa zamani amabao sasa hivi ni walimu na marefa wa mchezo huo Said Chaku(52) atazipiga na Jocky Hamisi(58), pia Bakari Dunda atazipiga na
Baina Mazola
No comments:
Post a Comment