Katibu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Mkoa wa
Tanga(Chadema) Jonathan Bawehje amemuagiza Katibu wa Chama hicho Jimbo la
Korogwe Vijijini,Salim Sempori kumuandikia barua Mwekezaji wa Shamba la Mkonge
la Kwashemshi Estate awalipe fidia wakazi wa kijiji cha Kwashemshi
walioharibiwa mazao yao waliokuwa wamepanda kwenye shamba hilo ndani ya siku
saba la sivyo watakwenda kumshtaki mahakamani.
Athumani Rashid, mkazi wa Kwashemshi akizungumza na uongozi wa Chadema Tanga |
Mkutano unaendelea. |
Agizo la Katibu huyo alilitoa kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika juzi kwenye kijiji cha Kwashemshi na kuhudhuriwa na viongozi
mbalimbali wa chama hicho akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya
Korogwe,Dastan Mndolwa.
Hatua hiyo ilitokana na wananchi wanaoishi baadhi ya
maendeleo yanayozunguka shamba hilo
ambao walikuwa wakilima mahindi kila mwaka bila kuwepo kwa usumbufu wa aina
yoyote lakini wakashangazwa na hatua ya mwekezaji huyo msimu huu kuharibu
mahindi ambapo baada ya wao kupanda mahindi alikwenda kuyafyekea chini kitendo
ambacho kimewapa wakati mgumu wakulima hao.
Mkutano ukiendelea. |
Aidha Katibu huyo alilaani kitendo ambacho kilifanywa na
mwekezaji huyo kwa kuharibu mazao ya wakulima ambao walijitolea kwa nguvu zao
kwenda kulima wakitegemea watapata mazao badala yake wameharibiwa na kuzitaka
mamlaka husika kulichukulia uzito suala hilo
ili waweze kupata haki zao za msingi.
Alisema madhara yaliyopatikana ni makubwa sana na yanarudisha nyuma maendeleo ya
wananchi hao na kuwataka kuwa imara kuweza kudai haki zao kwa kufuata utaratibu
uliopo kwani wanawajibu wa msingi kufanya hivyo.
“Diwani ameshindwa
kuwatetea wananchi kwenye maeneo yenu nasema hivi sisi kama chadema
hatutaki
mchezo lazima tuwapeleke mahakamani wale wote wanaohusika na suala hilo
ili iwe fundisho kwa vyama vyengine na kama noma na iweze noma “Alisema
Bahweje.
Akizungumza kwenye mkutanoi huo,Mmoja wa wananchi wa eneo
hilo,Mwanaidi Mussa alisema wao kama wakulima walifuata taratibu zozote
zinazostahili lakini wanashangazwa na kitendo kilichofanywa na mwekezaji huyo
ambacho wana kifananisha kama cha kinyama.
Katibu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, mkoani Tanga, Jonathan Baweje, akijadiliana jambo na viongozi wa chama hicho Kata ya Kwashemshi, kabla ya kuanza mkutano wao wa hadhara. |
Akizungumzia suala hilo,Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mrisho
Gambo alisema tatizo hilo wamelisikia kuhusiana na wananchi wao kuharibiwa
maeneo yao kwa taarifa za awali walizozipata eneo hilo ni la mwekezaji ambapo
wananchi wanapewa kwa ajili ya kulimo kwa kuchangia sh.10,000 kwa shughuli za
kilimo kila msimu.
Gambo alisema wao kama serikali watamuita mwekezaji pamoja
na viongozi wa kata ya Kwashemshi kuzungumza nao ili kuangalia namna gani
wananchi wa eneo hilo
wataweza kufaidika na maeneo hayo.
“Tutamuita
mwekezaji na viongozi wa kata ya kwashemshi
tuzungumze nao na mwisho wa siku tuangalie
tunafanya nini ili wananchi wanafaidika kwa kiwango kikubwa kwenye eneo hilo na
kama mwekezaji anapaswa kufahama kuwa anapokuwa na wananchi lazima angalie
namna ya kuhangaika nao lakini hawezi kumfukuza mtanzania kama anamfukuza mbwa
“Alisema DC Gambo.
No comments:
Post a Comment