BARAZA la Wazee wa Klabu ya Yanga, limetangaza kufanya
maandamano makubwa siku ya Jumatatu ya Machi 17, endapo Manispaa ya Ilala
itashindwa kuwajibu ombi lao la kuongezewa heka 11 katika eneo la Jangwani ili
wajenge Uwanja wa kisasa wa michezo, kwa madai kuwa wanazunguushwa na wanawekewa kauzibe na serikali hiyo waliyofanikisha maendeleo yao tangu kuasisiwa kwa klabu hiyo.
Maandamano hayo yatashirikisha wanachama na wapenzi wa Yanga,
kwa madai kuwa serikali imeshindwa kuwathamini na kutotambua mchango wao, licha
ya klabu hiyo kujihusisha na mambo mengi ya kimaendeleo, hivyo wanaona ni fursa yao sasa kuanza kuitisha maandamano hayo makubwa.
Endapo maandamano hayo yatafanikiwa, huenda ikawa timu ya kwanza kuandamana kwa kuishinikiza serikali, huku wakitambua kuwa nchi hii inaongozwa kwa mujibu wa sheria na sio kulazimishana.
No comments:
Post a Comment