Na Kambi Mbwana, Aliyekuwa Handeni
KATIBU wa timu ya vijana
wenye umri chini ya miaka 18 ya Lyons Sport ya kijiji cha Komsala, wilayani
Handeni, mkoani Tanga, Sadiki Mbwana, amesema kwa kuwekeza kwenye soka la
vijana, mpira wa Tanzania unaweza kupiga hatua kubwa.
Sadiki Mbwana, pichani.
Akizungumza mjini humo, Mbwana alisema kuwa jambo hilo
limewafanya waendelee kuweka mikakati ya kuiendeleza timu hiyo ya vijana,
inayotokea katika mgongo wa timu kubwa ya Men Stone.
Alisema kuwa kwa kulifanyia
kazi jambo hilo, wanaamini mchakato huo utakuwa
na mashiko, hivyo wanaendelea na mikakati yao
kuliboresha kwa kuiunda timu hiyo vizuri.
“Naamini huu ni mpango mzuri
ambao kwetu sisi utakuwa na mafanikio makubwa, jambo linalotupa moyo zaidi.
Timu za vijana zianzishwe
katika kila mahala, tukiwamo sisi tunaopatikana katika wilaya, ukizingatia kuwa
ndio sera yenye tija kwa soka la Tanzania,” alisema.
Kwa mujibu wa Mbwana,
wanaamini kwa kuiendeleza zaidi timu yao ya
vijana, wanaweza kukuza soka la wilaya yao ya
Handeni na Tanzania
kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment