Na Revocatus Mathias, Dar es Salaam
MWENYEKITI wa Soka Mkoa wa Iringa Sprian Kuamba amewapa
viatu wachezaji wa timu ya Lipuli inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, ili kuwapa morali kuelekea mwishoni mwa Ligi
hiyo.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam, Kuamba alisema kuwa amefikia hatua hiyo baada ya timu hiyo kupoteza
mchezo wake dhidi ya Majimaji ya Songea na kwmba zawadi hiyo iwe chachu ya
ushindi katika mechi zote zilizobaki ili kuhakikisha timu yao inapanda na kuwa
katika timu zitakazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.
“Ili timu
yetu iweze kusonga mbele inahitaji jitihada ya hari ya juu hasa wakati huu
tunapoelekea mwishoni mwa ligi hii ambapo mechi tulizobakiza ndizo zitakazo
amua timu yetu inaingia katika ligi ya Vodacom au la, hivyo zawadi hizi ni
chachu ya kuhakikisha tunashinda mechi zetu zote tulizo bakiza”,alisema.
Timu hiyo ilipoteza
mechi yake mwishoni mwa wiki iliyopita kwa kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka
kwa timu ya Majimaji ya Songea, na kusema kuwa
zawadi hizo ni kuwatia moyo wachezaji ili wacheze kwa kujituma katika
mechi zao zote zilizobaki kabla ya Ligi hiyo kumalizika.
Lipuli FC
inashuka dimbani leo katika uwanja wa Majimaji ili kuwania pointi tatu na timu
ya JKT Mlale, na baada ya mechi hiyo watajiandaa kuikabili timu ya Pongezi
kutoka Mafinga kabla ya kumalizia Ligi hiyo na timu ya Bukinafaso kutoka
Morogoro.
No comments:
Post a Comment