Na Mwandishi Wetu, Dodoma
KAMA ilivyotarajiwa na wengi, Bunge la Katiba limeahirishwa
tena mchana wa leo hadi hapo saa 10 jioni baada ya mvutano wa wajumbe na Kamati
ya Kanuni kuendelea. Mwenyekiti wa Muda wa Bunge hilo, Pandu Ameir Kificho,
aliwataka wajumbe kujiandaa hadi sioni ili wapitishe kanuni hizo.
William Lukuvi, Mjumbe wa Bunge la Katiba
Awali mjumbe wa Bunge hilo, David Kafulila, alimtaka
mwenyekiti wao kuhakikisha kuwa Bunge hilo linasitishwa hadi mvutano wao
utakapomalizika ili kuokoa posho zinazoendelea kutafutwa bila kufanyiwa kazi.
Wakati hayo yanaendelea, kila mjumbe alikuwa akifanya
vituko, ikiwamo kuwasha kipaza sauti na kuzungumza bila kupewa ruhusa na
mwenyekiti wake.
Mjumbe mwingine wa Bunge hilo, William Lukuvi, aliwajia juu
baadhi ya wajumbe wengine akisema kuwa wamekwenda Bungeni kuzomea. “Naomba
niseme kitu kimoja, wengine hatuogopi kuzomewa, tumeshazomewa sana hivyo
hatuogopi.
Endeleeni kuzomea lakini lazima niseme maana wanaozomea ni
wale wale wa siku zote, hivyo katika hili lazima tujuwe kuwa wananchi
wanatushangaa kwasababu hatufanyi kazi iliyotuleta hapa,” alisema Lukuvi.
Kauli yake iliibua zogo zito, hivyo mwenyekiti wa muda
kuwataka wajumbe kuwa makini na kuacha kuzungumza bila kupewa ruhusa.
No comments:
Post a Comment