Na Mwandishi Wetu, Muheza
MKUU wa wilaya ya Muheza ,Subira Mgalu, pichani, amesema wilaya hiyo
imeanzisha doria za mara kwa mara kwenye maeneo ya misitu na ukanda wa bahari
kwenye kata za Kigombe ili kuweza kukabiliana na wimbi la uharibifu wa
mazingira hususani ukataji wa miti.
Mgalu alitoa kauli hiyo wakati akisoma taarifa fupi ya
wilaya hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu Chiku Gallawa wakati
alipofanya ziara wilayani humo kwa kuzindua na kukagua miradi mbalimbali ya
maendeleo.
Alisema wilaya hiyo pia imewaondoa wavamizi waliovamia
misitu ya Kwani na Tongwe ikiwemo kupandwa miti ipatayo 1,500,000 ya matunda
,kuni,kivuli na viungo iliyopandwa kuwa kushirikiana na wadau mbalimbali
hususani shule,mashirika binafasi kwa ajili ya kuendeleza hifadhi ya mazingira.
Aidha aliongeza kuwa kumekuwa na uharibifu wa tatizo la
uharibifu wa mazingira na ukataji miti unaochochewa na mahitaji ya ardhi kwa
ajili ya kilimo,mbao kwa ajili ya samani na maeneo ya kulishia mifugo.
Alieleza kuwa licha ya kulishia mifugo kumekuwa na uchimbaji
haramu wa madini katika msitu wa asili wa amani ambapo serikali imechukua hatua
mbalimbali ili kudhibiti tatizo hilo
la uharibifu wa mazingira.
Mkuu huyo wa wilaya alisema wameanzisha kampeni dhidi ya
athari za moto na kufanyika vijiji 32 vilivyo karibu na misitu ili kunusuru
bionuai ikiwemo kuhamasishwa wananchi kufanya shughuli za ufugaji wa nyuki na
upepo ambazo ni rafiki wa mazingira pamoja na kuendelea kutoa elimu juu ya
umuhimu wa misitu na athari za uharibifu wa mazingira.
Hata hivo,Mgalu alizungumzia suala la migogoro ya ardhi kwenye
wilaya hiyo alisema mingi kati ya hiyo inahusu uvamizi wa mashamba makubwa ya
mkonge ambayo hayaendelezwi ipasavyo pamoja na mipaka ya wilaya inayohusiana na
vijiji vilivyopo mipakai ikiwemo mashamba saba ya mkonge,shamba la mifugo
lililopo Azimio na shamba la mifugo Mivumoni.
Aliongeza kuwa mgogoro uliopo kati ya Muheza ,Tanga na
wilaya ya Pangani hatua za kuuupatia ufumbuzi unaendelea kushughulikiwa katika
ngazi ya mkoa na ule kati ya wilaya ya Muheza na Pangani mazungumzo kati ya
uongozi wa wilaya hizo mbili bado yanaendelea ili kufikia muafaka.
No comments:
Post a Comment