https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Sunday, March 16, 2014

TFF yalalalamikiwa mkoani Tanga

Na Mwandishi Wetu, Tanga
BAADHI ya Wakazi waliokuwa wamejenga katika eneo ambalo shirikisho la soka nchini kwa kushirikiana na shirikisho la soka duniani (FIFA) wanatarajiwa kujenga uwanja wa Kimataifa wamelalamika kuwa serikali bado haijawalipa fidia ili kuweza kupisha ujenzi wa uwanja huo.
 
Hatua ya wakazi hao inatokana na kuona Rais wa Shirisho la soka nchini (TFF)Jamali Malinzi akitembelea uwanja huo na kuanza mikakati ya ujenzi wa uwanja huo ambao unatarajiwa kugharimu mabilioni ya fedha za kitanzania.
 
Wakizungumza katika nyumba zao wanazoishi ndani ya eneo la shirikisho hilo lililopo Mnyanjani jijini Tanga baadhi ya waathirika hao ambao wengi wao ni akina mama Christina Lucas alisema wamekuwa wakihangaikia fidia kila kukicha kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ili waweze kupisha ujenzi wa uwanja wa kimataifa bila mafanikio yoyote.
 
Alieleza zaidi kuwa baadhi yao wameshapewa maeneo ya kwenda kujenga nyumba baada ya serikali skuridhia ombi lao lakini fidia ndio imeshindwa kutoka hadi wakati huu kitendo ambacho kinawaweka kwenye wakati mgumu.

Naye Zabila Iddy alisema wanaiomba serikali kuharakisha zoezi hilo ili shirikisho la soka la kimataifa Fifa kwa kushirikiana na CAF na TFF waweze kuanza ujenzi wa uwanja huo haraka iwezekanavyo.
 
Hata hivyo akizungumzia suala hilo,Mjumbe wa kamati ya utendaji
TFF,Khalid Mohamed alisema tayari taratibu za kuwalipa zilishafanyika kwa waathirika hivyo watawasiliana na viongozi wa serikali ili kujua zoezi hilo limefikia wapi.

Jitihada za kumpata mkuu wa wilaya ya Tanga ili kuweza kuelezea
malalamiko hayo ya waathirika ambao wamedai wamekuwa wakifika kwake mara kwa mara bila mafanikio zinaendelea.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...