https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Wednesday, March 05, 2014

Pitia maoni mbalimbali ya wadau wakijadili tatizo la maji wilayani Handeni katika group la Handeni Kwetu kwenye mtandao wa facebook

Februari 26 mwaka huu mwaka huu kwenye group linalojulikana kama Handeni Kwetu lililopo kwenye mtandao wa facebook kulikuwa na mada tata ya tatizo la maji wilayani Handeni, mkoani Tanga na Tanzania kwa ujumla. Na haya ndio maoni yaliyochangiwa na wadau mbalimbali kwenye group hilo.
 
SWALI LA LEO: NAOMBA AJIBU KAKA MENGI IBRAH MABEWA ILI NA SISI TUJIFUNZ KUTOKA KWAKE.
Kwako kaka Mengi Ibrah Mabewa, nimekuwa nikifuatilia sana nyendo zako kwenye mtandao na kuona unayo hadhina ya weledi katika kichwa chako. Bila kujua unaishi wapi, unaishije, naomba utusaidie au kutupanua mawazo yetu...

Unafikiri nini kifanyike ili kutatua tatizo la maji linaloendelea kuwa wimbo wa Taifa kwa Wilaya ya Handeni na kwingineko? Kila siku maji. Kila siku maji. Miaka inakwenda n...See More

 • Mengi Ibrah Mabewa Asante sana kaka Kambi Mbwana kwa heshima hii mimi kwanza ni mzaliwa wa Morogoro niliekulia Dar es salaam na maisha yangu yapo Dar es salaam,mzee Mhandeni Sonyo ni miongoni mwa walezi wangu.Baba yangu amezaliwa Kwa Mkono Handeni hivyo kwa asili ya karibuni mm ni Mzigua wa Handeni Tanga,Matatizo ya maji yanayoigusa wilaya ya handeni moja kwa moja yanaigusa familia yangu pia.Suluhisho la tatizo hili ni kuwa na mradi mkubwa wa mambo 3.Mosi kutoa maji ya mto wami mpaka Handeni hili ndilo suluhisho kubwa kuliko masuluhisho mengine yote.Nilitegemea kwa uwezo,akili na umaarufu wa mbunge wetu mràdi huu pamoja na changamoto zilizopo za gharama lakn kwa kutumia uzoefu na nafasi aliyonayo serikalini na kwa wahisani inawezekana kabisa mradi huu ulafanikiwa.
  Jambo la pili ambalo mimi naamini inawezekana kabisa likifanyika linaweza kumaliza tatizo la MAJI handeni ni Kuwa na mradi mkubwa wa kuchima visima virefu ktk maeneo ambayo yanauwezekano wa kupatikana maji kwa kushirikiana na world Bank project au fedha za ndani has a ukizingatia handeni katika bajeti zote huwa either hawawekwi kwenye bajeti au hupata fedha ndogo ktk sekta ya MAJI.Chili pia litategemea kiongozi aliepo ana ushirikiano kiasi gani na viongozi wenzie waliopo katika sekta husika.
  Jambo la tatu ambalo Mimi ningekuwa kiongozi ningelifanya ili kupunguza au kuondoa kabisa shida ya MAJI ningeiga mfano wa morogoro KWA kujenga bwawa kubwa kabisa na kuelekezea vyanzo vote vya MAJI kwenda katika bwawa hilo.
  Nahili linawezekana likafanywa na halmashauri yenyewe kwa kujipangia mipango yake ya mud a mrefu hata miaka mitatu na kwa fedha zake,ruzuku ya serikali kuu,bajeti ya wizara ya MAJI au kukopa kwa bank za ndani kwa rasilimali ilizonazo wakiwemo wafadhili wa ndani ya wilaya,wadau na wawekezaji.
  Naamini hay a yakifanyika tatizo la maji litakuwa historia.Wamasai nyikani wameweza,CHALINZE wameweza sembuse sisi?
  Mungu ibariki Handeni na watu wake.
  Ahsanteni kwa ushirikiano KWA pamoja tutaweza
 • Kambi Mbwana Eheeee? Hope unaendelea kushuka kaka Mengi Ibrah Mabewa kwa mujibu wa comment yako ya chini, inaonyesha inaendelea.........
 • Kambi Mbwana Mfumo huu kama nilivyosema unaweza kuwa endelevu kama sisi wadau wenyewe tutauridhia. Kwangu ni mzuri. Unapanua mawazo yetu zaidi. Watakaotajwa ni wale member ambao wapo active sana, yani wanaonekana mara kwa mara, wakilike au kuchangia mada zinazokuwapo katika group hili. Badala ya kusubiri mada kisha tukosoe, tunataka kujua vichwani mwetu tunawaza nini? Akili zetu, zinaweza kuwa mkombozi wa Taifa, ukizingatia kuwa mitandao ni sehemu muhimu ya kuelimishana na kupashana habari. Baada ya Mengi Ibrah Mabewa kushusha mawazo yake hapa, bado tutakuwa na watu wengine muhimu ambao nao tutawaomba watuelimishe kwa namna moja ama nyingine. Jamani, tunaweza kuendelea ku comment kulingana na anachokisema mtajwa wetu hapo juu. Tupo wengi sana humu na kila mmoja atatajwa tu, akiwamo Hussein Sendaro King Gwanggaeto, Oumar Obs Bin Sebo, Gumbo Saleh Mhita, Hassan Kisabya, Rashid Hassani Kilo, Mhandeni Sonyo, Yasin Mohamed, Doyo Hasan Doyo, Mimi Hemed, Mashaka Mhando, Sanura Ali, Prince Rajah, Jerome Mhando na wengineo weeeengi tutakaowaomba wafanye hivyo..
 • Mathew Kiongozi Naomba na mimi nichangie kama naruhusiwa Kambi Mbwana
 • Majuto Kingama Kaka MBWANA naomba bro. MENGI HAJAMALIZIA MAELEZO YAKE HAPO. CJUI NN TATZO. KWANGU MIE HAJAKATA HATA ROBO YA KIU YANGU YA KUCKIA MTAZAMO NA USHAURI WAKE KTK HII Water crisis! inshort cjauona u-active wake!
 • Kambi Mbwana Majuto Kingama, bado hajamaliza mdau. Huwezi jua anatatizo gani, labda amekwama kwenye shughuli zake. Si unajua wengi wapo kwenye majukumu yao? Kwanza nilimshtukiza sana, hope anatumia muda huu kuweka anachojua katika eneo hili ili kila mmoja aelimike. Mengi Ibrah Mabewa namuelewa, akisema amemaliza atasema. Si unaona comment yake imekatika hapo juu? Aha ha ha haaaaa.. Kaka Said Mdoe na wewe utakuwapo tu, lazima. Tena wewe ndio nakupendaga sana. Mkuu Mathew Kiongozi, upo wewe? Huu wanaita nusu mdahalo. Naona Kingama zamu yako ikifika patachimbikaaaa. Aha ha ha haaaa. Napenda sana.
 • Yasin Mohamed Kambi mbwana tatizo la maji handeni ni la kisiasa linalokosa weredi wa viongozi wetu,hivi unahabari singida tatizo la maji linaelekea kuwa historia? Kijiografia singida na Dodoma ni kukame sana, iweje singida waoneshe mwanga wa kulimaza tatizo sisi wa handeni tushindwe? Mto pangani ambao umepita korogwe na baadhi ya sehemu handeni, mto wami ulioko pwani pamoja na visima vya kisasa vya bei nafuu vingetosha kabisa kumaliza tatizo la maji handeni,.kinachotukwaza handeni ni viongozi na si vinginevyo.kambi nakuhakikishia wakitokea viongozi handeni wenye nia ya dhati ya kuikomboa handeni, tatizo la maji litabaki historia.kambi handeni kijiografia sio kukame mpaka tuwe na tatizo la kudumu la maji,handeni maji yapo ila viongozi hawana nia ya dhati ya kuwasaidia wanahandeni waweze kuyapata kwa urahisi.
 • Mathew Kiongozi Nipo kama sipo. Niko busy na wageni wetu wa kutoka Misri...Nitachangia zamu yangu ikifika Kambi Mbwana
 • Doyo Hasan Doyo @kambi mbwana huwa siku zote Mimi natoa ufumbuzi wa tatizo hili ila wenye mamlaka hawayatilii maanani Sana mfano niliwahikusema kuwa wananchi wawezeshwe miradi midogo ya kuvuna maji Kila mwenye nyumba ya bati yaan ajejgewe kisima kwa mkopo kisha baadaya muda furan anarejesha mkopo huo hii ninjia ya kwanza ambayo inawezekana kabisa watimize wajibu watawala na wananchi kero hii ya maji Handen itakuwa History mifano iko mingi sana Botswana swaztland Namibia kule mvua kwa mwaka inajyesha Mara mbili kwa kwaka au Mara moja lakin wadau hamuwezi a mini kwamba hakuna shida ya maji"Hatua ya pili kutoka mshwaha mpaka Handen
 • Kambi Mbwana Hapo sasa, Majuto Kingama, Doyo Hasan Doyo. Kaka Yasin Mohamed, wote nawasoma. Naona mambo ni mazuri sana aisee. Hivi ndivyo tunavyotaka iwe. Na Mashaka Mhando naye ajipange, tunamuhitaji aje kilingeni hapa. Aha ha ha haaa.
 • Doyo Hasan Doyo Mwisho wa siku haya yote ni maamuzi ya kisiasa nn hatma ya huu mjadala?
 • Hassan Kisabya nimechelewa ktk mjadala,ila nimefika nafuatilia comments zenu kisha nami nitatoa mchango wangu,hongereni kw fikra pevu
 • Mimi Hemed Serikali ni watu na watu ndio sisi. Hapa kumekusanyika watu wa kila aina. Nilichojifunza, mtoa mada anajua faida ya mjadala huu ni kujua namna gani tunaweza kuwaza na kufanikisha maendeleo. Pili eneo hili siku hizi linatembelewa na kila mtu, wakiwamo baadhi ya viongozi wetu. Tatu sisi member ni wazi tuna ukaribu na wengineo wenye mamlaka. Kama tulivyoona wengine wanavyokuwa wakali mtu wao anapolaumiwa, hivyo huyo anaweza kubeba kinachojadiliwa hapa na watu wao kupata cha kuanzia. Nne, tunasaidiana pia kukuzana uwezo wetu wa kufikiri kwa faida ya Tanzania. Mimi nimependa sana mfumo huu. Nausbiria kutajwa nione nawezaje kuchangia mada itakayopendekezwa, nikiamini kabisa ni faida kubwa kusoma au kusomwa na watu muhimu ukiwamo kaka Doyo Hasan doyo.
 • Sanura Ali Mjadala ni mzuri ndugu zangu kwanza unatusaidia kupanua mawazo,pili hata watu wa karibu wa mbunge wetu wanapitia na kusoma unaweza kusaidia wakapeleka mawazo kwa mkuu wetu yakapata ufumbuzi.
 • Doyo Hasan Doyo @wewe Hemed unaweza kuchangia haina shida karibu
 • Sanura Ali Sasa narudi kwenye mada.juzi nilisema mbwewe na mkata ni pua na mdomo,nikimaanisha karibu,sasa iweje wao hawana tatizo la maji?kikwete kabla hajakuwa mkuu wa nchi ndio aliyewapelekea maji.katowa wami.sasa ilitakiwa mbunge wetu anzie pale alipoishia mwenzie nae apeleke jimboni kwake.
 • Mimi Hemed Kweli kabisa dada Sanura Ali. Kumbe tunawaza pamoja? Vyema sana. Asante sana mkuu, Doyo. Nimeipitia comment yako hapo juu, nzuri sana.
 • Sanura Ali Yani mtu unaletewa tonge la ugali mpaka mdomoni halafu unasubiri mtu akwambie tafuna halafu meza mumeona wapi jamani.mungu katupendelea tuna wami, pangani,tuna milima,sasa itakuwa twmtafuta mungu ubaya
 • Sanura Ali Nilijaribu kuchimba kisima kidogo tu amani shule nikagundua maji hayapo mbali.zile pesa zetu za jimbo za mwezi mmoja tu angefumba macho angechimba visima japo vya pump ya mikono kila kijiji anghalau tungeshukuru japo shingo upande.angekuwa na pakujitetea.
 • Mengi Ibrah Mabewa Wadau naamini kazi mliyonituma nimemaliza naomba mnikosoe pale nilipokosea au kunipongeza pale mlipoona nimepatia nia ni kusaidia mawazo ya kuisogeza mbele wilaya yetu ya handeni.Karibuni
 • Majuto Kingama Kwa mtazamo wangu, ili kuweza kupata surulisho la kudumu la kuondokana na adha hii ya ukosefu wa maji safi na salama si tu kwa wananchi kuwezeshwa kukopeshwa kwa kujengewa matank au visima vya kuvunia maji yatokanayo na mvua. BINAFSI nauona mpango huo km ni wa muda mfupi sana na hvyo kuwa vgumu kufankiwa kuondoa adha hyo. Sana sana kaya ztakaweza kunufaika na mpango huo ni chache sana tena za mjini na co kwa watu wa vjijini. Embu tujiulze ili ukubwa kias gan cha tenk hlo ama kisima kitakacho chmbwa ili kukdhi matumiz ya kaya moja yenye watu 10 kwa kipnd cha muda wa kat ya miez 6- 8? Gharama yake itakuwa ni kiasi gani itakayoweza kuhumudiwa na mwananch wa kawaida asie na ajira, asie na kpato cha uhakika, anae tegemea milo 2 kwa siku usio na vìini lishe vya uhakika? Mwananch ambae wakat mwngne wkt mwngne anakosa hata mia 2 ya kununulia fungu la mchicha na badala yake kurumangia ugali kwa PICHA YA SAMAKI? inshort mpngo huo utaweza kuwanufaisha watu wachache 2 wny vjcent vyao. TUSITOLEE MFANO WA NCHI...looading..
 • Sanura Ali Ivi leo hata tusingekuwa na maneno mengi tungekuwa tunasema huku tunaona aibu .mfano wezetu wa jirani mtoto wa mkuu akisimama tu kapita.fadhila watakumbuka jamani.sasa sie kachelewa mabadiliko muhimu inatosha ndugu zangu.nina mengi ya kusema ngoja niwape nafasi wezangu.siishiwi maneno hapa.
 • Doyo Hasan Doyo @wewe Hemed tupo kwa maslaah ya Handen ndiyo maana tunaojesha njia watala wanna wajibu lakin pia RAIA tuna wajibu pia na hilo wadau tulijue
 • Hassan Kisabya Naamini TANGA,hususani Handeni tatizo la Maji ni la kisiasa,maana sidhani kama mito inatotiririka pale haitoshi kumaliz tatizo hilo,Mto pangani,Wami yote inapita Tanga,pia kuna vyanzo mbali mbali toka milimani,Ndugu zangu,tatizo ni kuwa (1) nchi hii imekuwa ni nchi ya chaguzi,kila jambo huanza kuonekana kama litafanyika wakati wa chaguzi tu,mimi nadhani ikiwa nchi hio itafanya chaguzi kila mwaka basi matatizo yote yataisha,leo hii ktk mitaa ndio barabara zinachongwa,lengo uchaguz wa serikali za mitaa,(2) tatizo ni ushirikishwaji,wananchi wa tanga hawashirikishwi ktk suala hilinachelea kusema kuwa nchi hii watu wamezoea kujifungia ofisini wakiwa na wanazoita kamati zao za chama wakitekeleza ilani zao kisha kuja na maamuzi yao kw jamii,na sio kukaa na wahusika na kupata fikra zao,naamini endapo wahusika watashirikishwa basi tatizo litakwisha kabisa,(3)serikali kuacha kutumia mifumo ya kichama ktk maisha halisi ya watu,maisha yachukuliwe ni muhimu kuliko mifumo,
 • Anna Joseph nimefurahishwa sana na mdahalo huu kwn unatupa changamoto sana ukweli handeni bila shida ya maji inawezekana kabisa kwn vyazo vipo vingi vyakumaliza hili tatizo sasa niwakati wa viongozi kuchukua hatua nimefurahi pia kwamchanganuo alioutoa kaka mabewa pia kaka kambi juhudi zako nazikubali sana
 • Doyo Hasan Doyo @kingama Fanya utafiti kabla hujasema mimi nimetoa njia mojawapo ambayo inawezakuounguza kero ya maji na unaposema Kuwa haiwezi kuleta tija hujafanya utatiti wa kutosha kwamsisi kulikuwa na shamba kubwa la pamba miaka ya Sabin kulikuwa na wafanyakazi said ya elfu kumi walikuwa na kisima kikubwa ambacho kiliwatosheleza wote na pia ikasukwa ways zakwenda uraian na maji yalifika pale kijijin nashida ya maji kwamsisi ilitoweka pili Handen kuna watu wenye visima yawajui kero ya maji kwamaana hao tayari wameondokana nashidayamaji na hoja iliyopo ninikirajyike ilikuondoa shida ya maji nafikiri wadau wamejielewa sina muda wa kujihizana lete kawazoyako@kingama
 • Kambi Mbwana Aha ha haaaa. Nimefurahishwa sana na majibu mazuri kutoka kwa kaka Mengi Ibrah Mabewa. Pia wadau wooote tunaoendelea kuchangia mada hii hapo juu. Shukrani pia dada Anna Joseph, mchango wako ni mzuri. Kaka Hassan Kisabya, umeeleweka sana. Kumbe inawezekana. Inawezekana kwasababu jamii ina hamu ya kuona matatizo haya yanakwisha..
 • Majuto Kingama .....kama botswana,namibia na swaziland. Hv ni vijnch vidogo vdogo mfano swaziland kiukubwa haina tofaut na wly yetu ya handeni uzuri ni kwamba wenzetu wapo makini na raia wao; SURULISHO LA KUDUMU: kuna aina tatu ili kupata ufumbuz wa kudumu wa hl tatzo. KWANZA NIWEKE WAZI TU KWAMBA JAPOKUWA MIE NI MZALIWA WA WA HAPA CHANIKA HANDENI KUTOKA KWA MAREHEMU MZEE HASAN MHINA KINGAMA NA MAMA YANGU BI TUMAINI MOSES. BABA AKIWA NI MGOSI WA SEUTA NAGONE NA MAMA AKIWA MNYAMBARA WA KULE MBEYA, HATA HVYO NMEISH ZAID UPANDE WA MAMA, MBEYA, DAR NA NJE YA NCHI HVYO NI MGEN WA MAENEO MENG YA WLAYA HII HATA HVYO hyo co 7bu ya kushndwa kuiona adha hii ya ukosef wa maj saf na salama. Hvyo bnafs naona surulisho la kudumu ni kwa serikal kuvuta maj kutoka mto pangan/korogwe na kutoka mbwewe yaje had mkata na kuja handen mjn. Kadhalika kuchmba na kuyaongezea ukubwa wa mabwawa yaliyopo lkiwemo bwawa kubwa la chanika na mabwawa mengne. Kuchmba visima vya pampu na vya umeme walau kisima kimoja cha pampu na ki 1 cha umeme kwa kila mtaa!
 • Yasin Mohamed kambi mbwana umefika wakati sasa wa handeni kuondokana na shida ya maji, mm kama mdau wa handeni nawashauri waheshimiwa hasa mbunge asome kwa makini maoni haya na kisha yanayowezekana ayatekeleze, na pia MASHAKA MHANDO ajifunze kupitia kwetu, tunakosoa kisha tunatoa ushauri sio yeye akiingia hapa jukumu lake kumsifia mbunge ili ajaze tumbo lake.
 • Kambi Mbwana Tatizo la maji Handeni. Ni kweli huu wimbo umekuwa ukiendelea kuimnbwa na mara nyingi hutumiwa kama kichocheo cha wagombea. Nina uhakika hata uchaguzi ujao wadau watatumia wimbo wa maji kama karata yao. Sasa basi, tunawezaje kufanikisha hili? Kweli jamii ishirikishwe. Wadau wenye nafasi zao washirikishwe pia. Ndugu zangu, ninachojua mimi, wapo wadau muhimu na wenye nazo sana. Hawa kwanza wavutwe na kuambiwa sera ya maji Handeni. Makampuni, mashirika, taasisi zenye kiu ya maendeleo zipo kibao. Hivi, kama mtu anaweza kuchezea milioni 1 kwa starehe zake, akiombwa kuchangia maendeleo au tatizo la maji atagomea? Watalaamu wanasema kiasi cha Sh Ml 700 zinaweza kukarabati miundo mbinu ya maji. Ml 700 ni nyingi, ila ni chache pia. Katika bajeti moja tu, inaweza kutengwa walau Ml 300 na nyinginezo kupata kwenye vyanzo vingine vya mapato. Wafanyabiashara wapo wengi sana Handeni. Kama wanaombwa wachangie mwenge, tuwaombe pia tushirikiane katika hili. Ofisi ya mbunge, ofisi ya Dc na nyinginezo hili ni rahisi kwao. Uchimbaji wa visima. Handeni ina vijiji 112. Means kuna visima 112 kwa haraka. Mtu mmoja anaitwa Mustafa Sabodo, anawasaidia sana wabunge wengine kuwachimbia visima. Ningekuwa mimi ningetumia pia njia hiyo. Ndio faida ya kujulikana. Ndio Cv inayoliliwa na watu wanaotaka madaraka serikalini. Maji yametoka Korogwe na kuishia Sindeni. Yani kuyatoa hapo tu hadi town tunashindwaje? Kuna mfuko wa jimbo. Kuna vyanzo kibao vya mapato. Na pia kuna watu wanaopenda kujitolea. Mzee Mohamed Mhita, yupo wapi aelezee namna gani walipata hisani ya kuiendeleza Handeni miaka ya nyuma, kabla ya uhusiano wao kuingia nyongo kutokana kugombea jimbo la Handeni mwaka 2005, 2010? Haya yote yanaweza kuwa na tija kama ushirikishwaji utakuwa mkubwa kama walivyochangia wadau wengine hapo juu. Mwaka jana kwenye tamasha, kuna mtu alinipigia simu, "Kambi nahitaji kuja kwenye tamasha, vipi nije na maji yangu au sasa mambo ni mazuri" Alisema mtu huyu. Nikamwambia maji yapo kaka. Nilimjibu hivyo kwasababu sikuwa lengo lake. Jamani tumechoka kudhihakiwa! Basi kila kijiji au Kata kiweke mikakati yake yenyewe kwa ajili ya kupambana na jambo hili.
 • Majuto Kingama Sawa#DOYA_HASAN_DOYA. nakubaliana na wewe kuwa hyo ni njia mojawapo ila c ufumbuz wa kudumu! Pia comment ya majbu yako kwangu ni tofauti na comment ulio itoa ambayo ndio kiini cha comment yangu yenye kupngana kias na mtazamo wako ktk kulpatia ufumbuz wa kudumu tatzo la maji 2lilo nalo!
 • Doyo Hasan Doyo Ni DOYO HassanDoyo @kingama
 • Mashaka Mhando Ha ha ha nacheka kisha nitakuja na data za visima alivyochimba Dk Kigoda na mpango wake wa maji ukoje pamoja na serikali. Handeni haina mto wa kudumu Msangazi zamani ulikuwa haukauki lakini sasa haupo.
 • Yasin Mohamed daaaaaah njaa itakuua mashaka
 • Rashid Hassani Kilo Japo niko busy kidogo, ila wengi twajuwa chanzo cha mto Pangani ni Mlima Kilimanjaro na mto huo umepitia sehemu moja iitwayo Kweisewa sina hakika na kudhani kwamba ni Kilometa ngapi kutoka Handeni mjini, Misima, Mzeri Ranchi ambako maji kutoka Kweisewa yamefika kwa jitihada za menejimenti ya Ranchi.

  Ila nitachangia vizuri nikitulia ila wanaofahamu umbali wa Handeni hadi Kweisewa wanipe faida.
 • Gumbo Saleh Mhita jamana wa kwetu mi ni wa Komoza, Vibaoni na Kilimilang'ombe kote huko nipo, hivi juzi nilikuwa Handeni nikafika Komoza aliko mama yangu bahati nzuri mashallah kwetu Bomba la maji limefika lkn nikauliza maji yanatoka? nikaambiwa sasa hv ni miezi hatuna maji nikauliza sababu nikaambiwa pump ya kuyasukuma hayo maji sijui kutoka wapi nimesahau eti imeharibika, nikawaambia subirini kipindi cha uchaguzi watalitengeneza tu hili bomba na maji yatatoka,.. Ok achana na hilo, swala la maji kama walivyochangia wadau waliotangulia suluhisho lipo lkn ni mipango ya wawakilishi wetu tu ndio inatufelisha kimaendeleo hakuna zaidi nna uhakika kila linaloandikwa hapa wanaliona wawakilishi wetu na hivyo vyanzo vya maji mlivyosema vyote wanavijua kwa sababu ramani ya Handeni pia wanayo mpaka wanaweza kuwa na migodi wakaiuza kwa mabilioni ya pesa basi lazima itakuwa wamefanya survey nzuri tu ya wilaya ya Handeni. Cha kufanya ni kuleta mapinduzi ya demokrasia Handeni lkn mkibaki kulalamika ishu ya maji humu na kuonesha vielelezo ya vyanzo vya maji vilipo tutasubiri jibu jingine tena zaid ya lile lilijaa midomoni mwa wana wa Handeni "mwonga hakoze njaze idibwawa?"
 • Yasin Mohamed nasubiri data kutoka kwa mashaka
 • Majuto Kingama Katikati ya maji, wana handeni tuna kiu,ni wachafu wa miili na mavazi! Lakn uzembe ni wa mbunge wetu alieshndwa kutuletea maji na kutuonyesha namna ya kuyateka. Kwahyo ingaweje kiu ni yetu sisi wanahandeni lakni uzembe ni wa mbunge wetu!! Hata hvyo tunapaswa kuwa wavumilivu na kutorudia makosa 2lyo yafanya kwa zaid ya miaka 20. Mwaka 2015 uwe mwsho wa adha hii. MABADILIKO NI SASA NA 2015 TUNAMALZA KAZI!
 • Sanura Ali Sawa bwana kaka majuto kingama tumekusoma.ila majibu tunayo sisi wanahandeni.2015 tuombe uhai na afya nje.kitaeleweka tu.
 • Mhandeni Sonyo Asante sana ndugu yangu @Sanura
 • Mengi Ibrah Mabewa Mimi nikiachana na Mh Mbunge niwaombe madiwani wetu wote wa Handeni watueleze katika bajeti yao ya mwaka 2014/2015 vipaumbele ktk MAJI ni nn na wametenga kiasi gani? Maana isijekuwa na wenyewe ni wasaliti tuu.
  Ukiacha mbunge ambae tupo nae Dar es salaam
 • Kambi Mbwana Hapo kwa madiwani mtihani mzito.. Migogoro ya ardhi na kero nyingi wengi wao wameshindwa kusimamia. Yani, ni hatari kaka Mengi Ibrah Mabewa...
 • Majuto Kingama Vema 2015 tukafanya mabadiliko ya kisiasa. Tuwajaribu na wapnzani tuone. Au mnasemaje bandugu?
 • Sanura Ali Bandugu kingama tumekuelewa hila linawezekana.ila mimi mtazamo wangu kwetu handeni naona kama bado.vyama vya upinzani tatizo hawaelimishi watu vijijini.so wananchi wa vijijini hawana muamko na vyama pinzani.sijui kama nimeleweka ndugu zangu.umenisoma kaka majuto kingama?
 • Majuto Kingama Dada #SANURA. wakongo hapo wanasema "WANA EZA PROBLEM" hilo ndilo tatzo. Hakuna vyama vya upinzan handeni ila kuna bendera,kanga,skafu na kadi za vyama za upnzan. Lakn hakuna ofcn wala viongoz. Achana na MAYOWE YA KAKA DOYO HASAN WA DOYO. AND IT I HURT SO MUCH! INANIUMA SANA HALI HII0 NAJPANGA KWENDA PALE UFIPA STRT. NINA JAMAA YANGU NIMESOMA NAE. NI MTU MZTO MZTO KDOGO. NTAMPA MCHONGO MZMA ILI KUONA ANAFKSHA KWA JUU! NI LZM TUWE NA VYAMA VYA UPNZAN VYENYE NA CO KUSUBIRIA HADI UCHAGUZ MKUU UKARIBIE NDO WATU WAANZE KUJPTSHA PTSHA!!
 • Mengi Ibrah Mabewa Tatizo lililopo si kujaribu viongozi au vyama vya siasa tatizo ni mfumo jamani tunachotakiwa kufanya ni uraghabishi kama huu na unaruhusiwa popote duniani ila nitashangaa sana kama kuna mtu atapingana na haya tunayoyafanya atakuwa ni mtu wa ajabu kabisa hasa akiwa kiongozi au mtu mwenye ufahamu wa mambo.
 • Doyo Hasan Doyo @kingama mbona unapamhana na Mimi hiyo ndiyo stail yako ya kujejga hoja nikuhakikishie huna uwezo wa kupamhana na Mimi kwahoja yoyote ile hiyo chadema ndiyo hiyo inakwenda kuzimu halafu Mimi jimefanya siasa Handen kijiji kwa kijiji huwezi kunilinganisha na mwanasiasa yeyote kwa Handeni na kwa stail yako huwez
 • Majuto Kingama Kaka #MENGI_IBRAH_MABEWA. uyasemayo ni sawa. Hata hvyo kumbuka kuna wanahanden zaid ya lak 3 na wenye uwezo wa kutumia social network ama waliomo ndan ya group hili kwa ujumla wake hawazid elfu 20. Sasa kuhusu hao wengne waliobaki? Nadhan ipo namna ya kufanya ili "KUAMSHA"
 • Mengi Ibrah Mabewa Majuto Kingama ndio kusema badala ya sisi kulalamika tuu ni lazima tuoneshe kitu kwa kufanya mambo kwa vitendo ikiwa ni pamoja na kuelimisha wananchi juu ya kuhoji maendeleo yao ikiwemo bajeti wanayopangiwa hiyo ndio kazi ya kuwa MRAGHABISHI
 • Majuto Kingama Hahahahaha #DOYO_HASAN. don't panic ! Sina mpango wa kupambana na wewe pia mie si mwanasiasa ila ni mwanaiarakat wa mabadiliko ya kisiasi,kiuchumi na kijamii. Ngojea ninkunong'oneze mambo haya ma 2, marehemu mzee kingama wakati wa uhai wake aliwah kuniambia nyny watu wa upinzan kpnd kile upo cuf hususan wewe kuwa wanasiasa wazuri wenye kujua kujenga hoja na kuzitetea, kuchambua,kuulza maswali sahihi na majasiri. Lakin aliwikukosoa kitu kimoja kwamba wkt mwngne mlikuwa mnatumia lugha chafu za matusi na kulazmisha mambo yenu kwa ku2mia "NGANGARI PALEPALE JINO KWA JINO VILE VILE" la pili 2 ni kwamba mie ni mjasiriamal ambae huenda sana unguja, na mara nyng hufkia pale bububu jeshni nyumba ya pili tu kutoka kwny nyumba ambayo ndio makao makuu ya ADC kwa unguja kaskazini. Kule wanakujua na kukuheshmu sana hata mie mwnyw nlijizolea UJIKO kuptia umaarufu wako. Hvyo cwez kukuvunjia heshma yako lakn pia achana na panic zczo na mcng! WE KIONGOZI MKUBWA BHANA!
 • Majuto Kingama Sawa,sawa kaka #MENG_IBRAH. hilo ndilo wazo langu. Lakn tutaanzeje anzeje bila ya kuwezeshwa? Manake tumezoea mambo hayo kufanywa na wanasiasa wa upnzani!
 • Rashid Hassani Kilo Nimepata muda kidogo, nimejaribu kupitia maoni mbali mbali ya wadau juu ya mjadala huu wa suluhisho la shida ya maji Handeni.

  Kama utaliangalia kwa upana wake tatizo hili litaondolewa na sisi vijana ambao kwa sasa tunaonekana kuvua sura ya uwoga na kuvaa joho la ujasiri ili kubadili uongozi hasa mbunge ikibidi hata chama kwani hata viongozi wa ccm ni tatizo wameshindwa kabisa kusimamia irani ya chama kwa aslimia nyingi tu.

  Naongoe hivi nikiwa na maana kama mbunge anashindwa kuwajibika wapi kamati ya maadili wilaya?
  Kama diwani ameshindwa kuwajibika, wapi kamati ya maadili kata? Hawa wote njama yao ni moja sababu mbunge ndiye aliyetumia pesa kuhonga wajumbe wanaopiga kura kupitisha watu wake ambao nao watampitisha wakati wa kura za maoni na hata kwenye uchaguzi mkuu wanakesha macho kuona anapita.

  Hivyo mbunge ni mtu mkubwa sana anauwezo wa kuidhibiti wilaya au jimbo, sasa wakati umefika hapa tulipofishwa tuseme imetosha! Sina ugonvi na chama cha mapinduzi ila akitokea mwingine sina tatizo.

  Jamani Kwamatu hadi Sindeni maji bwelele hapo Halmashauri ya mji kipindupindu na homa za matumbo, mwaka 1 uliobaki ni rahisi kuliko kuchimba bwawa na kusubiri mvua.
 • Kambi Mbwana Hapo ndio tatizo aisee. Kwamatuku, Komsala, Sindeni maji yapo. Kutoka Sindeni hadi Misima na Handeni tunashindwaje kufikisha maji mjini? Hili ni tatizo kubwa, Siku moja nilipitia bwawani Handeni nusu nianguke kwa presha. Jamani, jamani, hali ni mbaya.
 • Kambi Mbwana Inawezekana sana tatizo la Panya litakwisha kama paka atafungwa kengele! Tatizo ni nani wa kumfunga paka kengele? Na Panya watakuwa wa ajabu sana kama wanaamini kuna siku paka atajifunga mwenyewe kengele! Aha ha haaaaa. Huu msemo mzuri sana...
 • Oumar Obs Bin Sebo Kaka #Kambi na wadau wengine nimekuwa nje ya mtandao leo muda mrefu ndo kwnza nabisha hod mda huu, nimekuta mada nzur ambayo inaendelea kujadiliwa msijal tupo pa1 ni majukum tu yalinibana kwa cku nzima.
 • Kambi Mbwana Sawa sawa Oumar Obs Bin Sebo. Mada ilifunguliwa na kaka Mengi Ibrah Mabewa kwa utaratibu mzuri wa kutaja mmoja wetu na kupewa mada au kuombwa kuchangia mawazo kwa anachoona kama njia ya kutafuta suluhisho. Na sisi wengine tujiandaye. Nyie ni watu muhimu sana. Tunahitaji kujua vichwa vyetu vinawaza nini? Vina uwezo wa kuchangia kwa maendeleo yetu? Isije ikawa ni wepesi wa kulaumu wakati kiutandani hatuna tunachojua au tunachoweza kutenda...
 • Sanura Ali Sasa kupitia madahalo huu nimejifunz kitu muhimu sana.mtaniuliza nini?jibu ni kwamba tukiamua kwa pamoja ,kwanguvu zetu wote na mungu akitusimamia tunaweza kuikomboa handeni.hapa sisi hatupambani na mtu au chama,bali tunataka handeni tuikomboe itoke kwenye mfumo hasi tupate mfumo chanya.vijana,wazee,kina mama ,kinababa imefikia wakati tusilale tena tuamke.njia nyeupe.haina makorongo wala hakuna wakutusumbua .
 • Rashid Hassani Kilo Dada Sanura,
  Ni kweli kabisa hapa hatugombani na mtu wala chama, ila upo msemo mmoja wa kizigua unasema; "NYOKA INENGILA MWEDIBIGA WATULANYA NEDIBIGA" Maana nyoka akiingia kwenye mtungi, kumuuwa lazima uvunje na mtungi!

  Ni wakati wa kutafuta tatizo kabla ya kutibu tatizo!
 • Mimi Hemed Safi sana wachangiaji wooote.
 • Mhandeni Sonyo Kambi wewe umepita bwawani sisi ndo tunaishi hapo. Ndo maana tunalalsminka
 • Juma Goda wadau hili swala la maji handeni imekuwa ni tatizo. bado haifahamiki litaisha lin?
 • Mhandeni Sonyo Halikwepeki na yeyote atskakuja iwe priority namba moja
 • Mhandeni Sonyo @Majuto hapa ni kuwa na mpango mkakati/Strategic plan ijadiliwe na wananchi na wadau wote kstila kila kata na baadae iwasilishwe kwenye halmashauri. Kutokana na umuhimu wa tatizo la maji ni muhimu kuwahusisha wadau.
 • Mengi Ibrah Mabewa Kambi Mbwana au Rajabu Athumani tunaomba tupate nakala ya bajeti iliyopitishwa na Halmashauri mana hiki ni kipindi cha bajet tuone halmashauri imepanga nn juu ya swala la maji kata kwa kata ili tuone analosema Mhandeni Sonyo tunaanzaje mana ni wazo zuri ila tunaweza kulaumu kumbe Halmashauri imekuja na mpango mzuri
 • Kambi Mbwana Yap ndugu Mhandeni Sonyo, nimepita bwawani kwasababu siishi Handeni, japo naenda mara kwa mara. Hapa kwenyewe nimerudi wiki iliyopita. Pia naishi vijijini, sisi ndio wale tunaosikia shida ya maji kwa wenzetu kwasababu kijiji chetu kina maji ya kutosha tu, naizungumzia Komsala. Kwa wale wasiojua, Komsala, Kwamatuku na Sindeni maji yapo, yanayotoka Korogwe, chini ya mradi wa Maji Korogwe... Na bili yote tunailipia huko...Kaka Mengi Ibrah Mabewa, nimelipokea...
 • Rashid Hassani Kilo Habari za asubuhi waungwana wote humu ndani!

  Kwanza nimpongeze kaka MENGI IBRAH MABEWA kuwaomba wanahabari wetu KAMBI na RAJAB wafanye kila linalowezekana waione badjet ya mwaka huu ya Halmashauri ya mjini na vijijini ktk upande wa maji tu, @mtaa na @kata tuone madiwani wetu walichokipanga juu ya suala la maji.

  Upande wa kata ya Misima sina shaka hakuna propozo yoyote juu ya maji kwa kuwa ubalozi wa Japan umefadhili milion 301, kwaajili ya bwawa japo lililochibwa si bwawa ila ni rambo ambalo hata ww usiejuwa unaona kabisa thamani yake haifiki hata milioni 150.

  Lakini kipo kijiji cha wafugaji cha MSOMELA ambacho bwawa lake lilibomolewa na maji kiasi cha kuwafanya wafugaji hao kusambaa kila sehemu kutafuta maji, ambao baadhi yao ni wale waliopatwa na kadhia ya kuchomewa maboma yao huko Mswaha kwaajili ya kufuata maji mto Pangani.

  Hivyo kaka Kambi na kaka Rajab, kwakuwa fany yenu ndilo jicho la wanyonge fanyeni ziara kwenye vijiji mione kero pengine zipo ambazo ni common kuliko maji japo najuwa tunakwenda na kero mojamoja na nini kifanyike.

  Kwani zipo kero nyingi kama kero ya ardhi-Kata ya Misima. Huduma za afya Hospital, vituo vya afya na Zahanati. Kutafanyika mikutano vijijini tuone FEDHA ZA RUZUKU YA MAENDELEO YA SERIKALI ZA MITAA (LGDG) zinafika vijijini nakufanya kazi iliyokusudiwa?

  Sijilaumu uwepo wangu humu ndani kwani vichwa vilivyomo humu vinanifanya niongeze upeo ktk elimu yangu ya drs la VII.
  ASBH NJEMA!
 • Mhandeni Sonyo Asante sana. Maji ya komsala sindeni nk ni maji yatokanayo na mradi wa maji Handeni yaani Handeni Trunk Main HTM na makao yake ni kijiji cha Tabora Korogwe na unatakiwa ujiendeshe wenyewe ukisaidiwa na Halmashauri ya Handeni. Bomba la mradi hu linatoka hapo Tabora, Kwamatuku mpaka Handeni njia nyingine ni inaenda mpaka Mazingara na Manga mpakani na Pwani. Mradi huu ulijengwa miaka ya 70 wakati wa mbunge wetu mpendwa mmarehemu Seuta wetu Musa Masomo. Kama mnavyoona mradi huu umezeeka.tatizo liingine watu wameongezeka vijiji sasa ni vingi na bomba limtoboka sehemu nyingi. Haya maji ya msingi Handeni. Kinachotakiwa ni kuufanyia ukarabati hii HTM. Lakini naungana na Mengi wetu Mabewa. Tufahamu je kuna mpango mkakakati Handeni kama upo unsemaje. Ninahisi mpango wa maji upo na unampa jeuri Mashaka Mhando kaujua kutoka kwa anaempa ugali. Bajeti ya mwaka huu na ujao ina mpango wa maji isijekuwa kama kawaida mabilioni lkn hakuna linalo fanyika. Handeni ilishapewa pesa za maji na serikali ya Japan zikalwa hivi hivi walpobanwa Tume ya Bunge wakasema wamejenga bwawa Kideleko jamani lipo? Kamati haikuliona. Bado tuna changamoto.
 • Mhandeni Sonyo Kama alivyosema ndugu yetu@Rashid Kilo tufikirie njia nyingine kutoka Kweisewa kupitia Mzeri hadi Misima na kuja mpaka Konje na Handeni. Tuwe macho sana hata ule mradi wa HTM nasikia ulipataga pesa miaka ya 90 lkn zimeyeyuka. TUIWA NA MPANGI WA KUFUFUA HTM NA HUU WA KWEISEWA TATIZO LITAPUNGUA SANA. Wakati huo Wazigua tutasema gumbo mtakowe
 • Yasin Mohamed mashaka nimesubiri nimechoka data sijaziona.
 • Mhandeni Sonyo Mchumia tumbo huyo hana cha data wala nini
 • Kambi Mbwana Kaka Yasin Mohamed, nahisi hujalala usiku wa kuamkia leo unasubiri data kutoka kwa Mashaka Mhando! Ajabu! Nakushauri endelea na mambo yako. Hakuna cha data wala nini kutoka kwake. Tatizo anafikiri hatuna kazi za kufanya hadi tunashiriki katika mijadala hii. Wote tuna dhamira. Tuna mipango. Na tuna hamu ya kuona jamii inanufaika. Wajinga wanaweza kusema; sasa suluhisho la mijadala yao mitandaoni ni nini? Mimi najibu, suluhisho ni kufahamu udhaifu wetu na kujua namna ya kuukabili, ukizingatia kuwa wote tunajenga nyumba moja.... Kumbuka, kila anayemulika nyoka anaanzia mguuni mwake...
 • Kambi Mbwana Rashidi Hassani Kilo wewe ni moto wa kuotea mbali. Ni mtu muhimu sana. Nashukuru Mungu. Nimeweza kukutana na wewe mara kadhaa, Handeni mjini na nyumbani kwako Misima. Una kitu fulani ambacho ni maalum kwa Tanzania yetu. Jiamini kama unaweza. Jiamini kuwa upo juu kuliko walionunua wanavyolingia. Sijui kwanini Misima wanashindwa kukutumia aisee. Nimekupata vizuri sana... Kaza buti...
 • Mashaka Mhando Data nitazianika, naendelea kuzi-compeil, halafu nipo Njombe ila Jumapili nitakuwa Handeni, sitaki kubabaisha katila mjadala huu mtamu na nina amini wengi hapa, mnachokosa ni taarifa hampo Handeni kwa muda mrefu, kaka yangu Doyo simshangai katika uchangiaji wake wa mada hii, vuteni subra kwani kila mwenye kusubiri yu pamoja nae 'Allah', nitawajuza.
 • Mhandeni Sonyo Acha wewe @Mashaka nazisibiri kwa hamu
 • Rashid Hassani Kilo Ndugu zangu kazi yoyote ukiifanya na kutanguliza njaa, basi mwisho wa siku utadhalilika na hatiye hata kupoteza CV yako.

  Mimi nimpongeze sana Kaka Kambi na mtaona si mimi tu ninayempongeza kwa jitihada zake za dhati za kutukusanya kupitia tamasha letu lile la @mwaka ambalo yeye ni mratibu.

  Anajitahidi mno hata kuwatembelea watu katika vijiji nikiwemo mimi alishafika Misima japo bado nina shida nae kuja kuona miradi kata ya Misima na mengineyo kwani uwandishi wa habari ni mhimiri pia.

  Hebu waandishi muige toka kwake na viongozi nitoe wito kuwa msije jenga bifu nae kwani yeye anaishi Dar na haya anayoandika tunampa sisi wapiga kura wenu.

  Na wale mfanyao kazi kwa maslahi ya matumbo yenu, mkumbuke Da most of your family are here at vijijini. So linaposemwa jambo la kuwasaidia usilete ushabiki usio na tija!
 • Kambi Mbwana Nitakuja tena kaka Rashid Hassani Kilo Misima. Hapo ni nyumbani kwetu bwana. Nasikitikaa safari yangu ya juzi ilikuwa fupi, hivyo nikashindwa kutua hapo. Niliishia Sindeni kisha Komsala, ambapo kwenyewe niliingia usiku wa saa nne usiku. Tuendelee kushirikiana kwa hili. Napenda kujifunza kutoka kwa watu wote. Tamasha la mwaka jana lilikuwa na mikono ya watu wengi hata kwa kutumia mawazo yao.
 • Yasin Mohamed Naamini wana handeni tukiamua tunaweza, kauli hii inathibitishwa na jinsi tulivyochangia mjadala wa maji handeni, ushauri wangu kwa wadau tujiepushe na wachumia tumbo kama mashaka ambao malengo yao ni kupotosha ukweli wa handeni kwa maslahi binfsi, kila member wa handeni apigane kuisaidia handeni, tukumbuke kuisaidia handeni si mpaka tuwe vuongozi,tuwekeni mikakati kuhakikisha walau tunajitolea kwa vijisent tulivyojaaliwa tuchimbe hata visima viwili kwa mwaka kunusuru hali mbaya ya maji handeni,kambi mbwana na wengine tuhakikishe tunabuni utaratibu wa kuisaidia handeni kwa vitendo, tusiishie hapa fb.nipo tayari kuipigania handeni kwa hali na mali. MUNGU IBARIKI HANDENI [MJASILIAMALI yacn 0713420242]
 • Bakari Masukuzi Nawaombea Heri na mafanikio mema katika kufanikisha mjadala wenu wa maendeleo ya handeni na tanzani mungu awabariki sana
 • Yasin Mohamed tunashukuru sana bakari masukuzi
 • Mimi Hemed Bakari Masukuzi, usijitoe, na wewe inakuhusu hiyo
 • Mimi Hemed Mashaka Mhando, nina wasiwasi na wewe? Mbona unatofautiana na wenzako? Kwani unanufaika nini? Upo tayari kujidhalilisha bilsa sababu za msingii. Tehe tehe teheee.
 • Bakari Masukuzi tupo pamoja sana @hemede
 • Mashaka Mhando Mjini Chanika Dokta kachimba visima zaidi 25, malambo yamechimbwa Mkata, Manga, Kwasunga, Malezi, Kilimilang'ombe, Komkonga, Kwekona, Mazingara, Magamba, Sindeni, Kwemagome, nk Kwamgwe visima zaidi 10 virefu vimechimbwa.
 • Mashaka Mhando Kuna progamu ya umeme wa REA ambao kwa Tanga wabunge waliopata ni Kigoda, majimarefu na mntangi. Kwa Handeni unaenda vijiji vya Kwedikwazu hadi Luiye, Vibaoni hadi Bogolwa, toka Segera, Maili10 hadi Kwakombo, Kwamkono, Kweditilibe hadi Konje.
 • Doyo Hasan Doyo @Mhando nafikiri mada hujaielewa hapa tunazungumzia tatizo la maji wewe unaleta habari ya umeme
 • Kambi Mbwana Duh, duh nimeona data za kaka Mashaka Mhando nimezikubali. Ebwanaaa heeee! Ni hatari...
 • Mathew Kiongozi Nawaza tu wenzangu kama nikikosea mnisahihishe. Wakati tunafikiria ufumbuzi wa muda mrefu, kuna ambaye amefikiria pia uwezekano wa kuanzishwa mfuko wa maji ambao utachangiwa kwa njia mbalimbali kama halmashauri, wizara husika, wadau wanahandeni walio sehemu mbalimbali duniani, wafadhili na mashirika kama WaterAid? Mfuko huu utawezesha kila kata kujengwa tenki au matenki makubwa ambayo yatakusanya maji kutoka kwenye kaya kadhaa ambazo zitawezeshwa kama kaya za mfano au zikajwngwa nyumba bora za mfano zikavuna maji yakajaa kwenye haya matenki? Mradi huu ukimilikishwa jamii na ukaendeshwa kwa usaidizi wa miaka mitano au kumi tu tatizo limeisha. Nafahamu changamoto ya nyumba za bati lakini siku hizi zipo nyingi vijijini na zikiongezwa kadhaa za usaidizi kisha ikachimbwa mifereji mikubwa ya kupeleka maji kwenye haya matenki yatakusanywa maji ya kutosha na kuwekwa dawa watu watumie. Maji mengi ya mvua hupotea mvua zinaponyesha. Tungeweza kuyakusanya haya maji pia na kuyaweka dawa kwa sbb kwanza ndio maji wanayotumia wengi ndg zetu toka kwenye mabwawa asilia shida ni yakikauka mvua zinapokatika na usalama wake kiafya. Uchumi ni kikwazo na ndio maana uwezeshwaji ni muhimu. Mfano huu nautoa kwa sababu mimi wazee wangu pale home karibu na stendi ya chogo wamemaliza tatizo hili kwa kuvuna maji ya mvua. Kuna kisima cha lita 96,000 kikijaa wanatumia maji kwa miaka miwili hadi mitatu hata mvua zisinyeshe tena.
 • Yasin Mohamed nahuzunika sana ninaposoma data za mashaka, hasa pale anapotaja maeneo ambayo najua wananchi wanateseka sana kwa shida ya maji.eti komkonga, kwamgwe, mkata, huna hata aibu? wadau moyo wangu umethibitisha kuwa mashaka ni mchumia tumbo, anaacha maji anaingia kwanye umeme, bahati nzuri natokea maailikumi , kigoda katuahidi umeme tangu 1995 na mpaka leo bado,namshangaa eti anatumia porojo hiyo kama data.sikia ndg we endelea kuwadanganya wabondei wenzio lakin handeni tumeshabaini ukweli, wewe na kigoda wako wote mungu atawahukumu kwa mnayofanya.
 • Yasin Mohamed umbummbumbu wa mashaka mhando unanitia wasiwasi hata kwenye fani yake, sina hakika kama habari zake anazoziandika huwa anazifanyia uchunguzi wa kina, ndg ukusanyaji wa habar is like research, lazima ufanye utafiti wa kina kabla hujatoa hitimisho. MASHAKA UKIENDELEA NA KUTETEA JAMBO AMBALO SI LA KWELI DUNIA ITAKUHUKUMU.
 • Kambi Mbwana Aha ha haaaa. Nina wasiwasi...
 • Bakari Masukuzi Hata mimi sina imani mashaka data za maji yeye analeta kwenye umeme sasa tumueleweje?
 • Juma Goda mashaka kuwa makini na hizo data zako. unauhakika????
 • Doyo Hasan Doyo @mashaka hebu jaribu kututajia hivyo visima Mimi nipo Handen sijawahi kusikia hiyo idadi tena Nina kitabu cha mheshimiwa kigoda cha kazi zake za miaka kumi iliyopita namipango kaazi ya miaka kumi anayomaliza hebu tueleze hizo data umezitoa wapi?
 • Doyo Hasan Doyo @Yasin napenda sana comments zako lakin usitumie ukabila in Mbegu hatari sana kwa mustakbal wa Taifa kumbuka sote ni watanzania
 • Kambi Mbwana Mashaka Mhando ndio data zako zimekwisha? Yani ndio mwisho huo? Duh, kaka wakati mwingine kuwa makini kidogo ili kulinda heshima yako. Unapozungumzia umeme vijijini unakuwa na maana gani? Aha ha ha haaaa. Kwanza sio hoja iliyopo mezani. Pili, vijiji vingi vinavyostahili umeme wala hawapewi zaidi ya hadithi tu. Mwaka juzi mwishoni, WAKALA WA UMEME VIJIJINI REA, walitumia gharama kubwa kujibu makala yangu niliyoandika kwenye gazeti la Mtanzania. Zaidi ya magazeti mawili yalipewa full pg 2 kwa ajili ya kusherehesha ile makala yangu. Maneno ya REA, waliafikiana na mahitaji yangu. Katika hoja yangu, niliwalaumu REA kuruka vijiji vingi, hasa Komsala ambapo kijiji hiki kipo kwenye underline. Sheria za umeme zinasema kijiji kilichokuwa kwenye underline kinatakiwa kupewa kipaumbele kupewa umeme. Komsala wanapitwa na line mbili, moja kubwa inayotoka Moshi kuelekea Dar es Salaam kama sikosei. Na pia unapita njia inayotoka KOROGWE kupeleka umeme Handeni mjini. TATU, Kijiji hiki ni kikubwa. Kina nyumba nyingi za bati. Lakini hakuna jipya. Nenda kwa Masokola katibu wa Mbunge Kigoda. Namlaumu sana, hawezi kuacha KOMSALA, Kwakiliga kupelekewa umeme badala yake wanapeleka umeme maeneo ambayo yapo mbali na njia za umeme. REA walitumia zaidi ya Sh Milioni 10 kwa ajili ya kujibu makala yangu. Gharama za umeme kijiji kimoja kilichokuwa kwenye underline hazizidi milioni 7. Huu si ujinga? Mwaka huu nimeangalia bajeti za umeme vijijini Komsala haipo. Huu si upupu? Halafu anajitokeza mtu anaingiza siasa, umbea mtupu. Tafadhali sana, hapa sisi hatuna mchezo mchezo. Nipo tayari kulichapisha tangazo la REA pamoja na ile makala yangu ili tufanye marejesho. Kiongozi aliyelala hawezi kuleya maedeleo hata kidogo. Mashaka kaa kwenye hoja, tujadili maji na jinsi ya kuyatatua na sio kuingiza siasa zisizokuwa na kichwa wala miguu. Kwa bahati nzuri, tunayojadili haya baadaye huwekea mkazo kwa kuhoji wahusika. Nimeshafanya hivyo mara nyingi na nitaendelea kuhoji kwa ajili ya kupata ufumbuzi.
 • Mimi Hemed Duh; ebwanaa kaka Kambi Mbwana umefunguka vibaya sana aiseee. Sijategemea hilo kutoka kwako. Ningependa kuona hilo tangazo linachapwa hapa. Sasa kama wametoa pesa kulipia tangazo ambalo ndani yake wamekubaliana na mawazo yako, kwanini hizo hela wasingekupa wewe tu? Au wangepeleka zaidi kwenye huo mradi wa umeme. Aiseee fedha za seriksali zinaliwa sana jamani.
 • Gumbo Saleh Mhita napenda kusema huu mdahalo naufurahia na mnanifurahisha wagosi, mazi ni uhai HANDENI BILA KHANGU VYADAHIKA.
 • Rashid Hassani Kilo Unajua ili mtu akuheshimu basi anza kujiheshimu mwenyewe na kazi yako ili iheshimiwe lazima mwenyewe uiheshimu,

  Ninachojifunza kwa kaka Mashaka yy si mwandishi wa habari, ikiwa kama ni mwandishi wa habari basi na wa mbunge.

  Mwanahabari si mwanasiasa, wanahabari tunawaona hata vitani kwa maana wame risk maisha yao na kwenye ukweli kama humudu kaa pembeni si lazima uchangie mbona humu wapo wadau wengi tu na wametulia? Si kama hawana hoja ila wanajitambua.

  Kinachozunguziwa hapa si nani kafanya nini, japo huyo nani anadhamana kubwa na ikifika hapo pia tutasema kwani hata sisi data kama hizo tunazo kuna watu kawanunulia pikipiki, hayo si mema yake pia!?

  Ila tupo kero ya maji tu.
 • Bakari Masukuzi kelo ya maji handeni itakwisha lini?
 • Mhandeni Sonyo Mashaka Mhando katoa data ambazo amepewa na Mbunge. Naona visima ba malambo yamechimbwa kiholela bila mpango. Kama ni hivyo mbona bado kuna tatizo la maji kwenye sehemu nyingi zikiwemo hizo zilizotajwa. Mbona tunafanya mambo kishaghala baghala. Tuwe na mpango mkakati ambao sio siri wahusika na wadau wauone na wachangie. Hivi wataweza kutuambia wilaya na mbunge wamefanya nini kuhusu Handeni Trunk Main HTM. Tuwe wawazi wananchi wajue isije ikatokea kama bwawa la kideleko. KWA REA NAKUBALIANA LKN WIGO UONGEZWE VIJIJI VIONGEZWE LAKINI ISIWE KIHOLELA IWE KWENYE MPANGO MKAKATI WA HANDENI
 • Bakari Masukuzi nkangu handeni itendesa jamani chimuseni yuno kigoda hakuchifaha mbeyu kabisa
 • Mhandeni Sonyo Hivi kwa miaka yote tangu miaka ya 70 hatjapata msaada kwa ajili ys HTM? UKIBORESHWA MTARO HUU UTAIKOMBOA HANDENI SIO HIVYO VISIMA. Katika visima vilivyojengwa Chanika pengine ni kimoja au viwili tu ndo vinatoa maji machache lkn mtaro unasambaza maji mjini kote. Ukienda Chanika shida ya maji ipo pale pale.
 • Prince Rajah Napita tu jamani,wakubwa shikamoni...naenda nunua maji nioge...Vibaoni bomba ni mapambo tu....
 • Bakari Masukuzi labda uoge umande aka mnyuzu maji uyapate wapi@roja
 • Prince Rajah Hahahahahaaaa 2nanunua kaka ndoo mia4 had 5.
 • Bakari Masukuzi kwa wale wasio na uwezo atanunua ndoo ngapi?
 • Kambi Mbwana Siku moja Rojah Prince, akanipeleka bwawani kuangalia maji. Duh, ilikuwa hatari jamani. Ndio kwetu. Hatupadharau, ila tunahitaji kujipanga juu ya hilo. Kaka Rojah kuna mjumbe aliomba tufahamu bajeti ya maji iliyotengwa mwaka 2014 na 2015 kwa wilaya ya Handeni... Nadhani wewe upo huko, tunakuomba ulifanyie kazi na utupatie majibu yake...
 • Prince Rajah Bwawani maji ni bure ila hayajatibiwa....ila tunakunywa hvyox2 maana ndio yaliotulea hadi xaxa....
 • Mhandeni Sonyo Bwa ka Handeni lilijengwa 1956 sio na Kigoda na hslina matengenezo kwa zaidi ya miaka 50 ndo maana msji yake ni tope
 • Mhandeni Sonyo Sasa hizo data zs wapi ikiwa Vibaoni na Chanika hali ni tete
 • Majuto Kingama Jamani! Mie nahisi huyu jamaa,#MASHAKA_MHANDO, huenda anakabiriwa na tatzo la kutokujtambua
 • Mhandeni Sonyo Ni kwrli ndugu yetu Mashaka ni wa kumsikitikia maana hajitambui na kwa hakika sio mwanandishi halisi wa habari. Mbona wenzie akina Kambi na Rajah na Mngazija pamoja na kutishwa wako imara. Au pengine njaa nayo inachangia. Handeni twahitaji waandishi imara wataotuletea taarifa sahihi hata kama mbunge hazimfurahishi. Na isiwe mbunge huyu tu iwe kwa yeyote atakaekuja
 • Kambi Mbwana Haya jamani. Hoja ilikuwa ni maji, ila kuna mdau akaingizia kipengele cha umeme vijijini. wengineo tumeshalia sana juu ya suala la umeme vijijini. Nimepost tangazo la REA juu ya umeme vijijini na mipango yao baada ya kusoma makala yangu kwenye gazeti la Mtanzania. ilikuwa ni kupata kiongozi mmoja na kuwakumbushia Rea, mbona mmesahau ahadi yenu? Je, fedha za tangazo hilo zimekwenda na maji bila faida yoyote? Duh nchi yetu hii bwana...
 • Rashid Hassani Kilo Umeme huu nadhani ulilenga sana vijijini. Lakini chaajabu vijiji ambavyo ni stakhili kupata vimekosa, na badala yake kunufaisha mjini. Labda kama kuna kijiji kimefaidika sana basi japo sijatembea sana Handeni ila MZUNDU, kwa 99% kama sio 100% na pia nahisi sio bure lazima kuna namna.

  Ila kwa mfano Misima ukiona nyaya za REA kama ni watu saba basi watano ni wenye uwezo kifedha. Ila nadhani bado haijaja kama hoja tuijadili.
 • Kambi Mbwana Yap, hilo kuna mtu aliingiza aliposema analeta data nzuri kwetu tujifunze. Badala yake alitoka nje ya mada ya maji yeye akaingiza suala la umeme vijijini, akisifia. Sasa kwa bahati nzuri, hilo jambo linasua sua na maeneo mengi yanaachwa bila sababu za msingi. Rejea comments zote utang'amua jambo kaka Rashid Hassani Kilo..
 • Mhandeni Sonyo Nakibaliana na wewwe0 ndugu yangu@kilo. Ndio maana kila mara nasisitiza kuwa tuwe na mpango mkakati/strategic plan ili iwe dira yetu hii ya mambo kiholela matokeo yake ndio hayo mradi ubafika mahali unawafikia watano tu maji visima 25 Chanika pengine hakuna hata kimoja chenye maji. Miaka ya 50 kulikuwa nakisima Chanika kilikuwa kibaoka watu sana sasa miaka 50 na mbunge miaka 20 hamna kitu. Kweli kazi tunayo lkn tukaze buti tutafika na Akina Mashaka watafute ugali kwingine labda kwa Maji Marefu ambae ni swahiba wa mhe wetu
 • Majuto Kingama Me namjua hata mtu alie ongoza "KAMATI YA USHINDI" had dr. Kigoda akashnda ubunge kwa mara ya kwanza mwaka 1995. Dr. Kigoda, hakuwa mtu mwenye umaarufu wowote hapa handeni na hakuwa na uwezo wa kushawish wapga kura ili wampgie kura! Inshort ABDALA KGD uwezo wake wa kuwa kiongoz wa watu ni mdogo sana... Mara nyng ushnd wake unawategemea watu wengne akiwemo huyo jamaa MAJI MAFUPI!
 • Sanura Ali Kaka mhandeni sonyo na ndugu yangu majuto kingama.unaona sasa faida ya mdahalo,tumeweza kujua vitu vingi tunabadilishana mawazo ,kumbe mpaka maswahiba tunawajua?inapendeza tuombe uzima na afya njema kitaeleweka tu.
 • Majuto Kingama achana na kitaelewaka bali 2015 KITASANUKA TU! Mzee wng aliwah kutwambia mambo meng kuhusu huyo jamaa dullah kgd mbaya zaid ni jns alvyo msaliti na kuwa upande wa adui wkt baba alpokuwa kwny matatzo il-har mshua ni yeye ndie alie changia kwa 80% awepo hapo alpo hv sasa!
 • Majuto Kingama achana na kitaelewaka bali 2015 KITASANUKA TU! Mzee wng aliwah kutwambia mambo meng kuhusu huyo jamaa dullah kgd mbaya zaid ni jns alvyo msaliti na kuwa upande wa adui wkt baba alpokuwa kwny matatzo il-har mshua ni yeye ndie alie changia kwa 80% awepo hapo alpo hv sasa!
 • Majuto Kingama Kwahyo mie cshangai kuona akiwasalt hata wapga kura wake! MHIIIIIITA! UKO WAPI MZEE? JIANDAE, 2015 TUNAKUPA WEWE JIMBO NA WAKILETA MIZENGWE YAO, VUA GAMBA NJOO HUKU, VAA GWANDA, TUTAKUWA NA WEWE PAMOJA DAIMA!
 • Mhandeni Sonyo Asante sana@Sanura na Kingama. Sote tuwe pamoja. Ukweli unajulikana ila la muhimu maji jamani. Tuwe pamoja tuikomboe Handeni kutoka kwa walaji
 • Mashaka Mhando Wadau yote kwa yote tumuombe MUNGU atujalie ifike 2015 kuna watu wataona aibu HANDENI KWETU.
 • Majuto Kingama Wa kwanza utakuwa wewe kilaza wa kujkomba komba@MASHAKA MHANDO.
 • Mhandeni Sonyo @Kingama asante muhimu ni eatu kujipanga yuifanye kazi huyu sie Mungu bhanaa. Waganga njaa akina Mashaka Mhando achana nao hawsjui lolote wao ni kuimba wimbo ws kgda. Ninavyomfahamu mzee wetu Mhita sijui kama anaweza kuvaa gwanda twende nae hukohuko aliko kwenye magamba tutashinda na wengine wameshaanza humu fb. Penye nia ipo njia. MUNGU IBARIKI HANDENI NA MUNGU IBARIKI TANZANIA
 • Mhandeni Sonyo Hakuna aibu kama tuna tafuta haki yetu. Wewe hakika utasibika utshindwa hata kutusngalia usoni. Daa ya ukombozi ndio hii. Karibu Handeni Mashaka usikse huko Tanga ngoma ipo Handeni na kama wasemavyo Wazaramo ndugu zetu ngoma inogile.
 • Bakari Mkwayu loading..........
 • Mhandeni Sonyo Pole sana naona itakuwa wewe. Jitayarishe. The wind of change is coming to Handeni. Upepo huo wa mabadiliko haukwepeki. Tupendane tusikebehiane ili tuzidi kupendana hata yatakapotokea mabadiliko. MUNGU IBARIKI HANDENI
 • Mhandeni Sonyo Huyu mwenzetu tumsamehe hajui anachofanya ila kumtukuza anaye mpa ugali hata kama sisi wote tunateseka. Hivi haoni sisi sote tunalalamikia yeye anasema Chanika eti kuna visima 25 yeye yuko Tanga sisi tupo Handeni. Tumpe pole kwani yeye sio sehemu ya jamii tunaoteseka. Sijui siku kutakapotokea mabadiliko atamsalimia nani. Maana tunajijua tunaopigania haki Handeni yeye anatutukana
 • Mhandeni Sonyo Mwenzetu Mashaka Mhando nina maanisha
 • Kambi Mbwana

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...