Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKUU
wa Wilaya ya Handeni, mkoani Tanga, Muhingo Rweyemamu, amesema kwa sasa ana
mikakati kabambe kuhakikisha shule zote za sekondari wilayani humo, zinashiriki
mashindano ya mpira wa miguu ili kuendeleza vipaji vyao.
Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu, pichani.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam, Rweyemamu alisema hali hiyo inasababishwa na wingi wa vijana wenye uwezo wa kucheza
soka, ila wanakosa misingi imara ya kuwaendeleza.
Alisema
baada ya kuwafuatilia kwa makini vijana mbalimbali, amebaini ili iwe na tija,
kuna ulazima wa kuhakikisha kuwa watoto wanaanzia hatua ya chini kabisa kucheza
soka.
“Nitazungumza
na wenzangu ili kuhakikisha kuwa nia yangu ya kuendesha mashindano ya vijana
kwa kupitia shule zote za sekondari inafanikiwa kwa vitendo.
“Naamini
mpango huu utakuwa na tija kwa kiasi kikubwa, ukizingatia kuwa tukiweza hivyo,
wanafunzi wetu watakuwa na mahala kwa kuonesha vipaji vyao,” alisema.
No comments:
Post a Comment