SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea amri ya Mahakama Kuu (Kitengo cha
Kazi) kukamata Sh. milioni 106 za klabu ya Yanga kutokana na mapato ya mlangoni
kwenye mechi zake ili kuwalipa waliokuwa wachezaji wake Stephen Malashi na
Wisdom Ndlovu.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam leo, Msemaji wa TFF, Boniface Wambura, alisema kuwa tayari
wameanza utekelezaji wa amri hiyo ambapo katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom
(VPL) dhidi ya Rhino Rangers iliyochezwa Machi 22 mwaka huu mjini Tabora wamezuia
Sh. 9,221,250 ambazo ndizo zilizokuwa mgawo wa Yanga katika mchezo huo
ulioingiza jumla ya Sh. 38,655,000.
Wachezaji
hao walifungua kesi kortini kupinga mikataba yao na klabu hiyo kuvunjwa bila
kulipwa haki zao za kimkataba. Malashi na Ndlovu walishinda kesi hiyo, hivyo
korti kuwapa tuzo hiyo ya sh. milioni 106.
Tunawakumbusha
wanachama wetu (klabu za Ligi Kuu, vyama vya mpira wa miguu vya mikoa na vyama
shiriki) kuzingatia mikataba wanayoingia na watendaji wao wakiwemo wachezaji,
makocha na maofisa wengine.
Iwapo
wanataka kuvunja mikataba ya ajira wafuate taratibu kwa vile hakuna mkataba
ambao hauelezi jinsi ya kuvunjwa iwapo upande mmoja unataka kufanya hivyo.
No comments:
Post a Comment